May 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Mkuu: Bukoba Vijijini ‘ngoma inogile’

Conchester Rwamlaza, amechukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Bukoba Vijijini kwa tiketi ya Chadema

Spread the love

WAKATI watia nia wanane kutoka CCM katika Jimbo la Bukoba Vijijini wakichuana kuwania kuteuliwa kugombea, Conchester Rwamlaza, aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (Chadema) tayari amechukua fomu. Anaripoti Danson Kaijage, Bukoba…(endelea).

Rwamlaza ambaye ni mgombea mwanamke katika jimbo hilo, ametamba kushinda kwa madai, chama chake kina wanachama wengi. 

“Licha ya watia nia wengi kujitokeza kwa upande wa pili (CCM), bado mtaji wa wanachama na mashabiki wa Chadema hapa ni wengi, hili linanipa matumaini,” amesema.

Akizungumza na MwanaHALISI Online muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge, amesema sababu kuwa ni kutaka kushirikiana na wananchi kufikia ndoto ya maisha yenye mwelekeo chanya.

“Jimbo hili lina vijana ambao kimsingi wanajishughulisha lakini hawana mtetezi wa kweli. Vijana wanalima ndizi, kahawa na wengine wanajihusisha na uvuvi, lakini wamekosa mtu wa kuwaunganisha kwa kuwatafutia miundombinu ya kujikwamua,” amesema Rwamlaza.

Jimbo hilo lilikuwa likiongozwa na Jason Rweikiza (CCM) ambaye anasema, idadi kubwa ya wanaojitokeza kugombea ubunge kupitia chama hicho, itafutika baada ya jina lake kupitishwa kuwania ubunge kwa awamu nyingine.

Rweikiza ambaye amekuwa mbunge kwa vipindi kwa vipindi viwili mfululizo, anaingia kwenye wakati mgumu baada ya idadi ya wanaCCM kutaka jimbo hilo.

error: Content is protected !!