Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi Mkuu 2020: JPM ‘Ukiniomba ruhusa nakupa lakini…’
Habari za SiasaTangulizi

Uchaguzi Mkuu 2020: JPM ‘Ukiniomba ruhusa nakupa lakini…’

Spread the love

WAKUU wa Mikoa, Wilaya na hata wakurugenzi wanaoomba ruhusa ya kugombea nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi mkuu ujao, wapo njia panda. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Ni baada ya kauli ya Rais John Magufuli, kwamba watapoomba ruhusa ya kwenda kugombea, watakuwa ‘wamejifuta kazi’ wenyewe.

Tayari baadhi ya viongozi hao wameoma ruhusa na kukubaliwa, lakini nafasi zao zimejazwa na wateule wengine huku Rais Magufuli akisema ‘nafasi hizo haziwezi kukaa wazi kuwasubiri.’

Rais Magufuli ameweka wazi msimamo huo leo tarehe 6 Julai 2020, wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni, Ikulu Chamwino, jijini Dodoma.

           Soma zaidi:-

Viongozi walioteuliwa ni na kuapishwa ni CP Thobias Andengenye, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma; Dk. Philemon Sengati, Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Mariam Mmbaga, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu.

Rais Magufuli amesema, ofisi ya umma haiwezi ikasubiri mtumishi ambaye ameomba ruhusa, wakati wananchi wanahitaji huduma yake, hivyo wakiondoka, haraka iwezekanavyo anateuwa watu wa kushika nafasi zao.

“Ili kazi ziendelee, taifa hili lazima liendelee na matatizo ya wananchi laizma yatatuliwe kila siku, hayawezi kusubiri mtu ameomba ruhusa mpaka ukarudi huko ruhusa ikishindikana, haiwezekani.  Huo ndio ukweli,” amesema.

Hata hivyo, amesema hawakatazi wateule wake kuomba ruhusa, bali anawataka waridhike na majukumu waliyokuwa nayo sasa hivi.

 

“Kwa wale wateule wangu ambao wachache wamekuwa wakiniomba ruhusa, nimekuwa natoa ruhusa haraka sana, yeyote anayejisikia kuniomba ruhsa hata leo, mnionmbe nitatoa. Kwa hiyo jamani ni ruhusa kila anayetaka kuomba nitampa,” amesema Rais Magufuli.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kuwaonya wateule wake, kutozikimbia nafasi zao, ambapo mara ya kwanza alitoa onyo hilo tarehe 22 Juni 2020, wakati akiwaapisha viongozi wa Arusha.

Rais Magufuli aliwaonya wateule wake wanaoomba ruhusa kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, akisema kwamba, hatowazuia kugombea bali watafakari kwa kina uamuzi wao na athari zake.

Akikazia onyo lake hilo, alisema hata kama wateule wake watafanikiwa kushinda katika kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitishwa kwao kutategemea na yeye ameamkaje.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!