September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Mkuu 2020: Rais Magufuli atangaza mapumziko Oktoba 28

Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura

Spread the love

RAIS wa Tanzania, John Pombe Magufuli ametangaza Oktoba 28, 2020 siku ya Uchaguzi Mkuu kuwa mapumziko. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo wa Rais Magufuli kuitangaza siku hiyo kuwa ya mapumziko, lengo ni kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu kuwachagua madiwani, wabunge na Rais watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.

Tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 na uchaguzi mkuu wa kwanza kufanyika 1995, uchaguzi umekuwa ukifanyika siku ya Jumapili lakini mwaka 2020, utafanyika Jumatano.

Gazeti la Serikali (GN) namba 30 la tarehe 24 Julai 2020 ndilo limetangaza mapumziko hayo yaliyosainiwa na Rais John Pombe Magufuli.

error: Content is protected !!