October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi mkuu 2020: Polisi Dar lawaonya wanasiasa, lasema…

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam nchini Tanzania, limewaonya wanasiasa kujiepusha na vitendo vya ukiukwaji wa sheria kuelekea maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Onyo hilo limetolewa leo Ijumaa tarehe 26 Juni 2020 na Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, wakati akizungumza na wanahabari jijini humo.

Amesema, watakaobainika kufanya vurugu katika uchaguzi huo, watachukuliwa hatua za kisheria.

Mambosasa amewataka wakazi wa Dar es Salaam hasa wanasiasa, kutii sheria za nchi ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani, kama Rais John Magufuli, alivyoagiza wakati anafunga shughuli za Bunge la 11 tarehe 16 Juni 2020.

Wakati anafunga bunge jijini Dodoma, Rais Magufuli aliwasihi Watanzania kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unafanyika kwa amani.

“Kwa wafuasi na wanawasiasa pia, maelekezo yalishatolewa na Rais Magufuli wakati anatoa hotuba kule Dodoma, alipokwenda kuhutubia na kuhitimisha Bunge, alisema Serikali iko macho kwa yeyote atakayejaribu kuufanya uchaguzi uwe wa haki na utulivu,” amesema Mambosasa

“Kwa maana ya mtu akifanya uvunjifu wa sheria atachukuliwa hatua, IPG Simon Sirro ametoa maelekezo pia, akielekeza wananchi wajiandae, kuhakikisha uchaguzi huu wa urais, wabunge na udiwani, unakwenda salama kama chaguzi nyingine.”

Aidha, Kamanda Mambosasa amewaeleza wanasiasa hawataweza kupata ushindi katika uchaguzi huo, kwa kufanya vurugu, bali watashinda kutokana na kupata kura nyingi.

“Hakuna atakayeshinda kwa kutengeneza vurugu, watashinda kwa ushawishi wao na kueleza sera zao kwenye kampeni, matokeo ya ushindi yatatokana na wingi wa kura, Dar es Salaam tuko vizuri tunashirikiana na wenzetu wa usalama kuimarisha amani,” amesema Kamanda Mambosasa.

error: Content is protected !!