September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Mkuu 2020: NEC yatoa ratiba fomu za urais, ubunge na udiwani

Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC)

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imesema, fomu za uteuzi wa wagombea urais wa nchini humo katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020, zitaanza kutolewa kuanzia tarehe 5 hadi 25 Agosti, 2020 ofisi za tume hiyo jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Hayo yamesemwa leo Jumatano tarehe 23 Julai 2020 na Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Semistocles Kaijage wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Jaji Kaijage amesema,  fomu za ubunge na udiwani zitaanza kutolewa tarehe 12 hadi 25 Agosti, 2020 ofisi za Halmashauri na Kata nchini.

          Soma zaidi:-

Amesema, uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 25 Agosti, 2020 na kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti hado tarehe 27 Oktoba 2020.

Kuhusu majimbo, Jaji Kaijage amesema, hakutakuwa na nyongeza ya majimbo na yatabaki yaleyale 264 ya mwaka 2015. Tanzania bara majimbo 214 na Zanzibar yako 50.

Jaji Kaijage amesema, kumefanyika mabadiliko ya majina katika majimbo matatu ambayo ni Chinolwa la Mkoa wa Dodoma kuwa Chamwino. Jimbo la Mtera pia la Dodoma kuwa Mvumi na Jimbo la Kijitoupele, Zanzibar kuwa Pangawe.

error: Content is protected !!