Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari Uchaguzi mkuu 2020: NEC yasema wapigakura ni milioni 29, vituo 80,155
Habari

Uchaguzi mkuu 2020: NEC yasema wapigakura ni milioni 29, vituo 80,155

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imesema idadi ya wapigakura katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28 2020 ni milioni 29 huku vituo vya kupigakura vitakuwa 80,155. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Idadi hiyo imetajwa leo Jumamosi tarehe 1 Agosti 2020 na Jaji Semistocle Kaijage, Mwenyekiti wa NEC katika kikao cha tume hiyo na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo.

Jaji Kaijage amesema, baada ya mazoezi mawili ya uboreshaji wa daftari la wapiga kura kukamilika, daftari hilo lina wapiga kura 29,188,347.

“Baada ya kutoa wapigakura ambao taarifa zao zimejirudia, kwa hivi sasa daftari lina wapiga kura 29,188,347. Kutokana na idadi hiyo ya wapiga kura kutakuwa na vituo 80,155 na kila kituo kitakuwana wapigakura wasiozidi 500,” amesema Jaji Kaijage.

Jaji Kaijage amesema, wapiga kura wapya ni 7,326,552 wameorodheshwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura, katika zoezi la uboreshaji wa daftari hilo awamu ya kwanza na ya pili.

Mwenyekiti huyo wa NEC amesema, idadi hiyo ya wapiga kura wapya ni sawa na  asimilia 31.63 ya wapiga kura 23,161,440 walioandikishwa katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015.

Katika mazoezi yote jumla ya wapiga kura wapya 7,326,552 waliandikishwa sawa na asilimia 31.63 ya wapiga kura wapatao 23,161440 walioandikishwa mwaka 2015.

Aidha, Jaji Kaijage amesema, wapiga kura 3,548,846 waliboresha taarifa zao katika daftari hilo huku 30,487 waliondolewa  kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kutokana na kukosa sifa kwa mujibu wa sheria.

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilifanyika kwa awamu mbili katika vituo 37,814, ambapo awamu ya kwanza ilifanyika tarehe 18 Julai 2019 na kukamilika tarehe 23 Februari 2020. Huku la pili, likifanyika tarehe 17 Aprili  hadi Mei  4 2020.

Akizungumzia mkutano huo, Jaji Kaijage amesema, NEC imewaita wadau wa  uchaguzi  ili kubadilishana nao mawazo juu ya namna ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi huo, ili kuepusha dosari zinazoweza kuathiri uchaguzi.

“Vyama vya siasa ni wadau wakuu na muhimu wa uchaguzi mkuu, kwani ndio wahusika wakuu wa uchaguzi, kutokana na ukweli huu, tume imeona umuhimu wa kufanya kikao cha pamoja ili kupeana taarifa na kufahamisha kuhusu maandalizi ya uchaguzi,” amesema Jaji Kaijage.

Jaji Kaigaje ameeleza, “vilevile, kikao hiki ni nafasi ya kubadilishana na kupeana uzoefu wa utekelezaji shughuli za uchaguzi ili kuepusha dosari zinazoweza kujitokeza na kuathiri shughuli za uchaguzi.”

Jaji Kaijage amewaeleza viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria mkutano huo kwamba, katika uchaguzi huu, hakuna marekebisho katika Sheria za Uchaguzi, bali NEC imefanya maboresho ya kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge.

“Ndugu viongozi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu hakukuwa na marekebisho katika sheria za uchaguzi, hata hivyo tume imefanya maboresho ya kanuni za uchaguzi wa rais na wabunge za mwaka huu na kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa,” amesema Jaji Kaijage.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!