Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uchaguzi mkuu 2020: Bosi Takukuru awaonya wafanyabiashara
Habari za Siasa

Uchaguzi mkuu 2020: Bosi Takukuru awaonya wafanyabiashara

Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) nchini Tanzania, imetahadharisha wafanyabishara kutojihusisha na vitendo vya rushwa, kupitia dhana ya ufadhili wa gharama za uchaguzi ndani ya vyama vya siasa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo amesema Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, leo Ijumaa tarehe 17 Julai 2020 wakati anafungua warsha ya wadau wa uchaguzi, kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya rushwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, jijini Dar es Salaam.

Brigedia Mbungo amesema, gharama za uendeshaji uchaguzi ndio chanzo cha vitendo vya rushwa, ambapo baadhi ya wafanyabiashara hutumia mwaya huo, kujinufaisha baada ya wagombea waliowafadhili, kupata uongozi serikalini.

“Lakini wapo wagombea wa vyama ambavyo vimekuwa vikichangiwa na watu wenye fedha na hasa wafanyabiashara ili kudhamini mchakato wa uchaguzi na baada ya uchaguzi watu hao wachache wenye uwezo hujipatia manufaa zaidi pindi wagombea hao wanapoingia kwenye madaraka,” amesema Brigedia Mbungo.

Brigedia Jenerali, John Mbungo, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru

Brigedia Mbungo amesema, kitendo hicho kinasababisha viongizi kufanya maamuzi ya kisera yenye maslahi kwa watu wachache.

“Mara nyingi chanzo kikuu cha rushwa katika uchaguzi ni gharama za uchaguzi. Jambo hili husababisha wagombea au watia nia kutumia ushawishi pamoja na nguvu ya fedha ili kurubuni wapiga kura wawachague. Mgombea au wagombea wenye uwezo wa kifedha, hutumia kigezo hicho cha fedha kuwarubuni wananchi ili wawachague,” amesema Brigedia Mbungo.

Kuhusu warsha hiyo, Brigedia Mbungo amesema, Takukuru imeamua kukutana na wadau wa uchaguzi, ili kuunga mkono azma ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ya kutaka uchaguzi huo unafanyika kwa haki, huru na usawa.

Mkurugenzi huyo wa Takukuru amesema, tarehe 16 Juni 2020 wakati Rais Magufuli anavunja shughuli za Bunge la 11, alisisitiza wadau wa uchaguzi waepukane na vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo.

“Ningependa tujikumbushe kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria kupambana na rushwa bila uoga wala upendeleo katika nyanja zote ikiwemo katika uchaguzi. Kwa kuzingatia katiba ya nchi inayoelekeza taasisi na vyombo vyote kuelekeza nguvu na juhudi kuhakikisha tunaondoa rushwa katika janii yetu, Takukuru imeelekeza nguvu katika hilo,” amesema Brigedia Mbungo.

Brigedia Mbungo amesema rushwa ina athari kubwa katika mchakato wa uchaguzi na kwamba ni lazima idhibitiwe.

Ametaja athari zake kuwa ni; wananchi kukosa viongozi wawajibikaji, waadilifu na wazalendo, uvunjifu wa amani kutokana na migogoro ya mara kwa mara ya kisiasa na taifa kugubikwa na rushwa.

Pia, rushwa inadidimiza uchumi wa taifa kutokana na ukosefu wa mipango thabiti ya maendeleo, kukosekana kwa uwazi katika maamuzi, utawala bora pamoja na wananchi kukosa imani na serikali yao.

Baadhi ya wahudhuliaji wa warsha hiyo ni viongozi wa dini, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania, Sisty Nyahozi na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!