August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi Meya Ubungo gizani

John Kayombo, Mkurugenzi wa Wilaya ya Ubungo

Spread the love

UCHAGUZI wa kumpata Meya wa Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaama unafanyika gizani, anaandika Pendo Omary.

Serikali imeagiza kwamba, waandishi wa habari wasiruhusiwe kuingia kwenye ukumbi wa uchaguzi na kuripoti.

Mwandishi wetu aliyeko Kibamba mahali zilipo ofisi za Manispaa ya Ubungo anaeleza kwamba, Msemaji wa Manispaa hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mariam ameeleza kuwa, ameagizwa kuwapa taarifa kwamba, hawaruhusiwi kuingia ukumbini.

Kwenye maelezo yake Mariam amesema kuwa, agizo hilo limetoka kwa John Kayombo, mkurugenzi wa manispaa hiyo.

Kwenye uchaguzi huo, Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimemsimamisha Boniface Jacob, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni pia Diwani wa Kata ya Ubungo (Chadema), naibu wake ni Ramadhan Kwangaya, Diwani Kata ya Manzese (CUF).

Idadi ya madiwani katika manispaa hiyo kutoka CCM ni watatu huku Ukawa wakiwa 18.

Mpaka sasa majina rasmi yatayoingizwa kwenye uchaguzi huo kutoka CCM bado hayajatajwa ingawa Yusuph Yenga na Kasim Lema wamekuwa wakitajwa na baadhi ya wajumbe wa CCM.

Tayari wajumbe wa mkutano huo wamefika eneo la tukio huku hali ikionekana kuwa shwari ikiwa ni pamoja na ulinzi kuimarishwa.

“Eneo linalozunguka ofisi na ofisi zenyewe lipo katika utulivu. Lipo gari moja la polisi (Defender) likiwa na polisi waziozidi 10,” anaeleza mwandishi wetu.

error: Content is protected !!