DONALD Trump, Rais wa Marekani amesema, uchaguzi mkuu nchini humo uliofanyika jana Jumanne tarehe 3 Novemba 2020 umekubwa na udanganyifu na kupanga kwenda Mahakama ya Juu nchini humo.
Rais Trump anayetetea nafasi hiyo kupitia Chama cha Republican, anachuana vikali na mgombea wa Demokratic, Joe Biden.
Akizungumza na wafuasi wake mapema leo Jumatano wakati shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, Trump amesema ameshinda uchaguzi huo ingawa bado mamilioni ya kura zilizopigwa hazijahesabiwa.
“Ukweli ni kwamba tumeshinda, uchaguzi umekubwa na udanganyifu” amesema Trump huku akisisitiza kwamba sheria lazima zifuatwe na “tutakwenda Mahakama ya Juu, kama upigaji kura utaendelea.”
Uamuzi huo wa Trump kutaka kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo, kutamaanisha mshindi akachelewa kupatikana.
Rais Trump amesema kinachotokea ni aibu “kwa nchi yetu.”
Mchuano bado ni mkali ambapo Biden anaongoza dhidi ya Trump katika majimbo yaliyokwisha kuhesabiwa kura zake na mchuano umejikita zaidi katika majimbo ya, Wisconsin, Pennsylvania, Arizona, Georgia na Michigan.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali kuhusu matokeo ya uchaguzi huo
Halafu eti wanataka kutufundisha Waafrika maana ya demokrasia. Huko kwao chaguzi zao zimejaa vurugu na tuhuma kibao. Wanasau boriti jichoni mwao. Huo ni ubeberu
Huko ndo kuna demokrasia ukiwa na wasi wasi unaenda mahakani kupata haki yakk sio huku bongo lala kwa huyu dikteta uchwara kwa wezi wasio na aibu