Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Uchaguzi Kenya: Raila na Ruto watofautiana kuhusu usajili wa wapiga kura
Kimataifa

Uchaguzi Kenya: Raila na Ruto watofautiana kuhusu usajili wa wapiga kura

Wafula Chebukati, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini Kenya (IEBC)
Spread the love

 

TUME huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya (IEBC), sasa ipo katika njia panda, kufuatia wagombeaji wawili wakuu wa urais katika uchaguzi mkuu wa 9 Agosti, ili kuwaridhisha wagombea wawili wenye nguvu katika uchaguzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Raila Odinga, mgombea urais  kupitia muungano wa Azimio One Kenya na William Ruto, anayetokea Kenya Kwanza, ambaye pia ndiye naibu wa Rais  wametofautiana kuhusu matumizi ya sajili ya elktroniki na ile ya kawaida (Karatasi) katika uchaguzi ujao .

IEBC ilisema haitatoa sajili za wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura na kusisitiza kutumia mfumo wa kielektroniki.

Huku Raila akisema, kuna haja ya matumizi ya rejista za kielektroniki na za karatasi za wapiga kura katika uchaguzi ujao, Ruto alionekana kuunga mkono  uamuzi wa  IEBC wa kutegemea sajili ya wapigakura wa kielektroniki pekee.

Katika hoja zake, Raila alitaka kujua ni kwa nini IEBC ilisita kutumia sajili ya wapiga kura iliyo kwenye karatasi.

Wakili wake, Paul Mwangi alieleza kuwa “hii ni kinyume na sheria ya uchaguzi.”

Alisema, kuwa sheria inaitaka tume kuwa na daftari la mwongozo la wapiga kura kama mfumo wa pili wa utambuzi wa wapiga kura endapo mfumo wa kielektroniki utafeli.

Raila Odinga

“Msisitizo sio kwamba usitumie teknolojia. Tumia mifumo yote ambayo imeelezwa lakini sheria inakutaka uwe na mfumo huo iwe utatumika au la,” Mwangi alisema.

Ruto kwa upande wake, amesema kuwa muungano wa Kenya Kwanza hauna wasiwasi na matumizi ya rejista ya kielektroniki mradi tu usalama wake umehakikishwa.

“Kumekuwa na ripoti kwamba Kenya Kwanza inataka sajili ya kawaida. Hatutaki rejista ya kawaida. Ukitupa ulinzi wa kutosha kwamba ya kielektroniki itafanya kazi bila uwezekano wowote wa kufeli basi sisi hatuna pingamizi,” alieleza.

Mgombea huyo alisema, matumizi ya vifaa vya kidijitali katika kuendesha kura ni njia katika demokrasia ya kisasa.

Katibu mkuu wa chama cha UDA, kinachoongozwa na Ruto, amedai kuwa daftari la wapiga kura linaweza kuweka njia ya udanganyifu kwa kuwafanya watu kupiga kura mara mbili.

Veronicah Maina, ameeleza kuwa rejista hiyo halisi inatoa nafasi kwa watu kuingia vituoni na kujifanya wanathibitishwa kutoka kwa usajili halisi ilhali hawajatambuliwa kupitia mashine maalum ya kilektroniki ya KIEMS.

“Kutokana na hayo, tuna wapigakura wengi ambao hawajajiandikisha wanaoingia kwenye vituo (vya kupigia kura), kupata karatasi za kupigia kura na kupiga kura kwa kukwepa kifaa cha KIEMS,” Maina aliongeza.

Tume huru ya uchaguzi na mipaka, ilifichua kuwa itatumia mfumo kamili wa upigaji kura wa kibayometriki katika uchaguzi huo.

Katika hali ambapo kitambulisho cha kibayometriki kitashindikana, maafisa hao watapitia Mfumo wa Kusimamia Uchaguzi wa Kenya (KIEMS), kwa kutumia nambari ya kitambulisho, ambayo itachukua taarifa za mpigakura ili kutambuliwa.

“Vifaa vya KIEMS hufanya kazi nje ya mtandao katika suala la utambulisho, inafanya kazi kupitia nakala mbadala. Maelezo haya yatakuwa katika kadi ya SD na ikiwa kuna hitilafu kadi ya SD inaweza kuwekwa kwenye kifaa kingine,” taarifa zinaeleza.

Taarifa hizo zitajumuisha alama za vidole za mpiga kura, ambazo zitampa nafasi karani wa uchaguzi kufanya upya kitambulisho cha alama za vidole ili kuthibitisha utambulisho wa mpiga kura.

IEBC imeeleza kuwa mbinu ya kusajili kwa mikono ina uwezekano wa kutumiwa vibaya ikisema wapiga kura wanapotambuliwa kupitia teknolojia, mfumo huo huweka kiotomati maelezo ya waliopiga kura kumaanisha kwamba ikiwa mtu huyo atajiwasilisha tena, basi mtu huyo hawezi kupiga kura (tena).

Kando na suala hilo la sajili ya wapiga kura mengine yaliyotolewa na timu ya Azimio ni utoaji wa orodha ya vituo vyote vya kupigia kura, muundo wa karatasi za kupigia kura na eneo la uchapishaji na idadi ya vifaa vya Kiems vitakavyotumika na nambari zao za mfululizo.

Timu hiyo pia ilihoji ni kwa nini wasimamizi kumi kati ya 47 wa kaunti wa tue ya uchaguzi wanatoka jamii moja.

Pia wanataka wapewe nakala iliyoidhinishwa ya sajili ya wapigakura, maelezo ya jinsi kadi za SD zitakavyopakiwa kwenye vifaa vya Kims na wafahamishwe eneo ambako tume ya uchaguzi itaweka makao yake ya kusimamia shughuli nzima ya kuhesabu kura.

Azimio pia ilitaka kujua ni kampuni gani itachapisha karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu. IEBC ilisema itajibu masuala yote ya kiufundi yaliyotolewa na timu ya Azimio na wagombeaji wengine wa urais wiki ijayo.

Naye Ruto, alieleza wasiwasi wake kuhusu masuala mbali mbali ya uchaguzi.

Mwenyekiti Wafula Chebukati, alisema timu yake imejitolea kuandaa majibu kuhusu masuala yote katika kongamano litakalofanyika mapema mwezi ujao.

Alisema kuwa tarehe itapangwa kwa wagombeaji wote wa urais kuzuru kiwanda kitakachochapisha karatasi za kupigia kura siku zijazo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!