January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchaghuzi Mkuu upo pale pale – NEC

Baadhi ya vifaa vya VBR Kit vilivyofika leo

Spread the love

HATIMAYE Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekata mzizi wa fitna. Inasema kuwa haina mpango wowote na wala haikusudii kuahairisha uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu, kutokana na sababu yoyote ile kama ambavyo inadaiwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Kauli ya NEC inaondoa hofu iliyotanda kwa vyama vya siasa, kwamba baada ya kushindwa kufanya kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa 30 Aprili mwaka huu, sasa inatengeneza mazingira ya kumwongezea muda Rais Jakaya Kikwete kwa kisingizio cha kutokamilisha uandikishaji wa wapiga kura. 

Akizungumzia mwenendo mzima wa uandikishaji wa wapiga kwa mfumo mpya wa Biometric Voters Registratin (BVR) unaoendelea mkoani Njombe, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amewaambia waandishi wa habari kuwa “hadi sasa tayari tumepokea BVR Kits 248.”

Amesema “NEC ilianza uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga katika mkoa wa Njombe 16 Machi, 2015, na sasa uandikishaji huo utakamilika rasmi 18 Aprili mwaka huu.”

Kwa mujibu wa Jaji Lubuva, uandikishaji huo, umefanyika kwa mafanikio makubwa katika kata zote za halmashauri ya wilaya ya Njombe Mjini na Vijijini, Wanging’ombe, Ludewa, Makete na Makambako.

Amefafanua kuwa, pamoja na kuahirisha kwa tarehe ya kura ya maoni ya katiba inayopendekezwa, NEC inaendelea na uandikishaji kwa kadiri ya uwezo wake kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha sambamba na kuendelea na kazi mablimbali kwa ajili ya kura ya maoni na uchaguzi mkuu.

“NEC inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu kuanza kwa awamu ya pili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mikoa ya Iringa, Lindi, Ruvuma na Mtwara ambalo litaanza 24 Aprili mwaka huu.

“Tume tayari imepokea BVR Kits 248 ambazo zinahitajika kufika mapema kuendeleza mafunzo, lakini leo tume inapokea BVR Kits 1,600 zinazokuja kwa ndege ya kukodiwa,” amesema.

Jaji Lubuva ameongeza kuwa, BVR Kits hizo zitatumika katika mikoa wanayoelekea kuandikisha na ifikapo 24 Aprili, wanategemea kupokea BVR Kits zingine 1,600.

Amesema “BVR Kits hizo zitawezesha kuandikisha katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Katavi na Ruvuma. Uandikishaji katika mikoa hiyo utaanza 2 Mei mwaka huu. Halikadhalika zitafuata BVR Kits 1,152 ambazo zitawezesha tume kufanya uandikishaji katika mikoa ya Singida, Tabora, Kigoma na Kagera katika tarehe itakayopanga baadaye.”

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, BVR Kits hizo zitagawanywa katika halmashauri ambapo itawezesha wapiga kura wote kuandikishwa ndani ya siku 28 kila halmashauri.

Hadi sasa Serikali imetoa dola za Kimarekani milioni 72 (Sh. bilioni 133). Kuwasili kwa mashine hizo, kunaifanya NEC kupokea mashine 2,098, huku ikisubiri mashine 5,902, ili kukamilisha 8,000 zinazotakiwa.

Vifaa hivyo vinanunuliwa na serikali kupitia kampuni ya Lithotech Export ya Afrika Kusini, ambayo imeingia mkataba na NEC na inaviagiza kutoka China.

error: Content is protected !!