July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uchafu kikwazo kwenye vivuko nchini

Spread the love

WAKALA wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) wameeleza changamoto mbalimbali inazovikabili vivuko nchini kuwa ni uchafu uliopo kwenye injini hivyo kusababisha mitambo kukwama, Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa Vivuko na Ukodishaji Mitambo, Mhandisi Japhet Massele alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema kuwa, suala la uchafuzi wa mazingira kwenye vituo vya vivuko hivyo husababisha takataka kuingia kwenye mitambo ambapo takataka hizo zina athiri mitambo hiyo na kusababisha kukwama kwa vivuko hivyo.

Mhandisi Massele ametaja sehemu ambazo zina matatizo yanayopelekea uharibifu wa vivuko hivyo ni kwenye kituo cha kivuko cha magogoni jijini Dar es Salaam, kanda ya ziwa ni utegaji wa nyavu kwenye njia za vivuko, kwenye mito ya Ruhuhu, Utete na Kilambo vivuko vinakumbwa na ukame na kujaa kwa machanga kwenye njia za vivuko hivyo.

“Serikali inataraji kuongeza vivuko vipya pamoaja na kuongeza cha magogoni\kigamboni licha kufanya ukarabati kwa vivuko vilivyopo,” amesema Mhandisi Massele.

Ametaja vituo hivyo 27 kwenye mikoa 11 ambapo miongoni mwayo ni Kivuko cha Magogoni/Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo hutumika kivuko cha MV. Magogoni, MV. Kigamboni na MV. Dar es Salaam.

Kivuko cha Utete/Nkongo mkoani Pwani hutumia Mv. Utete, Kivuko cha Msangamkuu/Msemo mkoani Mtwara MV. Mafanikio, Kivuko cha Ilunga/Kipingu mkoani Ruvuma MV. Ruhuhu, Kivuko cha Kyanyabasa/Baganguzi kutumia MV. Kyanyabasa na kivuko cha Rusumo/Nyakiziba hutumia kivuko cha MV. Ruvuvu Mkoani Kagara.

error: Content is protected !!