Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Tangulizi Ubunge wa Lissu: Hoja kuu 2 za mahakama, Mbowe ajitosa
Tangulizi

Ubunge wa Lissu: Hoja kuu 2 za mahakama, Mbowe ajitosa

Spread the love

MAHAKAAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi ya Tundu Lissu, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kutaka kufungua kesi ya kupinga hatua ya Job Ndugai, Spika wa Bunge kutengua ubunge wake. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Uamuzi huo umezingiatia hoja mbili zilizotolewa mahakamani hapo na Jaji Sirillius Matupa leo tarehe 9 Septemba 2019 kwamba;-

Mosi; Kuruhusu kufunguliwa kesi hiyo kungesababisha mgogoro wa kikatiba na kuwa, Jimbo la Singida Mashariki mwisho wake lingekuwa na wabunge wawili kinyume na Katiba ya Jamhuri.

Pili; Uchaguzi uliompa nafasi Miraji Mtaturu, kuwa mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), haujalalamikiwa na mpeleka maombi ambapo mahakama haiwezi kuhukumu kuhusu malalamiko ya uchaguzi huo ambapo sio sehemu ya madai ya mleta maombi.

Jaji Matupa amemshauri, hoja za waleta maombi mahakamani hapo (Lissu) ni nzuri na kwamba upade huo wa madai unawezak kurejea mahakamani kufungua kesi ya uchaguzi tofauti na mamombi ya sasa.

Lissu anaendelea na matibabu nchini Ubelgiji kutokana na kushambuliwa kwa 36, miaka miwili iliyopita akiwa anatoka kuhudhuria kikao cha bunge mjini Dodoma, risasi 16 zilimpata.

Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, alifungua maombo hayo kwa kwa njia ya uwakilishi unaofanywa na kaka yake, Alute Mughwai ambaye pia ni mwanasheria na wakili.

Katika shauri, Lissu aliomba kibali cha Mahakama Kuu ili afungue kesi ya kutaka uamuzi huo wa kuvuliwa ubunge, utenguliwe na arejeshwe kutumikia wananchi.

Ombi lake linamhusu Spika Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Spika Ndugai ndiye alitoa tangazo rasmi la uamuzi wa kumvua Lissu ubunge tarehe 28 Juni 2019.

 NJE YA MAHAKAMA

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa mahakamani hapo amesema, tayari Mahakama Kuu imefikia uamuzi wake na kwamba kwa bahati nzuri, nafasi ya kusonga mbele ipo.

Amesema, wao kama Chadema wanaheshimu uamuzi wa mahakama hiyo, na msimamo wa chama chake ni kuendelea kupigani haki ya Lissu.

“…ndugu yetu Lissu bado yupo nje kwa matibabu, tunatambua haki hii haiwezi kupatikana kirahisi…,” amesisitiza Mbowe.

Awali, Wakili Peter Kibatala, aliyeongoza Jopo la mawakili wa Lissu, aliiomba mahakama hiyo itoe amri ya kusimamishwa kwa muda kuapishwa kwa Mtutura kwa madai, kama ataapishwa kabla ya hatima ya shauri lake, itakuwa vigumu kupigania haki za mteja wake (Lissu).

Wakati huo jopo la mawakili wa serikali lililoongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Vicent Tango walipinga ombi hilo pamoja na mambo mengine wakidai, ombi hilo limekosewa kufunguliwa mahakamani hapo.

Walieleza sababu ya msimamo huo kwamba ni kutokana na kutumika kwa vipengele vya aya vilivyomo ndani ya kiapo, vilitupiliwa mbali na mahakama hiyo, hiyo vililikosesha nguvu ya kisheria katika shauri hilo.

Pia shauri lilifikishwa mahakamani hapo kwa nia mbaya ya kumkwamisha mbunge huyo mteule bila sababu za msingi.

Mawakili wa serikali walitahadharisha kuwa, kama mahakama ikitoa amri hiyo, itakuwa inaingilia utendaji kazi wa mhimili mwingine jambo ambalo Katiba haliruhusiwi.

Tayari Mataturu alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), baada ya tume hiyo kuendesha utaratibu wa kuziba nafasi aliyoiacha Lissu kufuatia uamuzi wa kuvuliwa ubunge.

Mteule huyo alitangazwa mshindi bila ya kupigiwa kura kwa kuwa ni pekee aliyerudisha fomu ya kuomba kugombea; waombaji wengine 12 wakitajwa kuwa hawakurudisha fomu zao.

Tazama video kamili hapo chini

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!