September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mapingamizi ya Serikali kesi ya Kafulila yatupwa

Spread the love

FERINAND Wambari, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora leo ametupilia mbali hoja za mawakili wa Husna Mwilima, Mbunge wa Kigoma Kusini na serikali dhidi ya David Kafulila ambapo waliwasilisha nyaraka za kurasa zaidi ya kurasa 3,00 kuomba kesi yake (Kafulila) ifutwe, anaandika Happiness Lidwino.

Katika hoja zao wamesema kwamba, hawaoni kesi ya kujibu baada ya Kafulila na mashahidi wake watatu pamoja na vielelezo kupokelewa mahakamani.

Akifuta hoja hizo leo mahakamani Jaji Wambari amesema, Husna anapaswa kutoa ushahidi uliompa ushindi lakini pia msimamizi wa uchaguzi huo naye anatakiwa kutoa ushahidi uliosababisha amtangaze Husna kuwa mshindi.

Baada ya kauli hiyo, Jaji Wambari ameahirisha kesi hiyo na kuagiza kusikilizwa tena tarehe 3 Mei mwaka huu.

Awali, Kafulila aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini aliamuliwa na mahakama hiyo chini ya Jaji Wambari kuwasilishwa mahakamani hapo, fomu halisi za matokeo ya uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kafulila alikubali na akaiomba mahakama kuiamrisha NEC kuwasilisha fomu hizo mahakamani ili ziweze kupitiwa kwa kulinganishwa na fomu alizowasilisha mahakamani. Awali Kenned Fungamtama, Wakili wa Serikali alipinga ombi hilo.

Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka jana, Kafulila inadaiwa kuwa ndiye mshindi lakini msimamizi wa uchaguzi alimtangaza Husna kutoka CCM badala yake.

error: Content is protected !!