January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ubunge Mbagala giza nene

Spread the love

MSISIMAZI Mkuu wa Uchaguzi katika Jimbo la Mbagala, Fortunatus Kagimbo ameshindwa kutangaza matokeo ya jimbo hilo kwa madai ya kutokuwepokwa maelewano miongoni mwa wagombea waliokuwa katika kinyanyaro hicho. Anaandika Faki Sosi … (endelea)

Ni siku ya tatu tangu wananchi wa Mbagala kupiga kura ya kuwachagua madiwani, wabunge na rais ambapo wananchi hao wameshindwa kupata matokeo hayo.

“Bado hatujapata maridhiano ya wabombea wa vyama vilivyoshiki uchaguzi huu ingawa leo tunaweza kutangaza matokeo ya ubunge katika jimbo hili, ” anasema Kagimbo.

Hali ya usalama katika kituo hiki cha matokea ya jimbo ilikuwa sio nzuri kutokana na wafuasi wa vyama vya siasa kutaka kupata matoko ya jimbo hilo ambapo askari wa jeshi la polisi walilazimika kurusha mabomu ya machozi kwa wafuasi hao.

Jimbo hilo ndio pekee jijini Dar es Salaam ambalo wagombea wa ubunge hawajatangazwa ambapo Jimbo la Temeke, Kinondoni, Segerea, Ubungo, Kawe, Kibamba, Ilala, Kigamboni na Ukonga tayari.

error: Content is protected !!