Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ubunge CCM: Askofu Gwajima, Abbas Tarimba wachukua fomu
Habari za Siasa

Ubunge CCM: Askofu Gwajima, Abbas Tarimba wachukua fomu

Spread the love

MAKADA zaidi ya 10 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, wamechukua fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo ya Kawe na Kinondoni. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mkwajuni, wanachama hao wamejitokeza leo asubuhi Jumanne tarehe 14 Julai 2020 wamechukua fomu kwa ajili ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kawe. Jimbo hilo lilikuwa linaongozwa na Halima Mdee (Chadema).

“Kwa sasa itoshe tu kwamba nimechukua fomu,” amesema Askofu Gwajima muda mfupi baada ya kuchukua fomu.

 

Kwenye foleni hiyo, alikuwemo Abbas Tarimba, aliyekuwa kiongozi katika Timu ya Mpira ya Yanga na Diwani wa Kata ya Hananasifu ambaye anaomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Kinondoni.

Mbunge anayemaliza muda wake kwenye jimbo hilo ni, Maulid Mtulia wa CCM.

Leo tarehe 14 Julai 2020, CCM imefungua pazia la uchukuaji fomu ndazi ya ubunge nchini. Zoezi hilo linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 17 Julai 2020.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online na MwanaHALISI TV kwa habari zaidi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!