Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ubinafsi, kutoaminiana vyatajwa mkwamo maridhiano kisiasa nchini
Habari za Siasa

Ubinafsi, kutoaminiana vyatajwa mkwamo maridhiano kisiasa nchini

Mwenyekiti wa Kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandara
Spread the love

 

KIKOSI kazi cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya siasa za vyama vingi imesema ubinafsi na kutoaminiana ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha maridhiano ya kisiasa nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumatatu tarehe 21 Machi 2022 na Mwenyekiti wa Kikosi kazi, Profesa Rwekaza Mukandara wakati akiwasilisha taarifa ya awali ya utendaji kazi wa kikosi kazi hicho kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu.

“Kutoaminiana kwa wanasiasa kunafanya mazungumzo na kufikia maridhiano kuwa ngumu katika nyakati tofauti…ubinafsi unaofanywa na baadhi ya wanachama wa vyama vya siasa kujali zaidi maslahi ya vyama vyao kuliko maslahi ya Taifa,” ameeleza Prof. Mukandara.

Mukandara ametaja sababu zingine kuwa ni kutokuwa na utaratibu rasmi wa kuwezesha maridhiriano ya vyama vya siasa pindi unapotokea mgogoro, vyama vya siasa na taasisi nyingine zinazihusika na masuala ya siasa na kidemokrasia kutokuwa na utaratibu wa kuelezana, kuelimishana na kujadiliana.

Pia ametaja sababu nyingine kuwa ni baraza la vyama vya siasa kutotekeleza majukumu yake ipasavyo mfano kutofanya vikao vya mara kwa mara.

Ili kuondokana na mkwamo huo Kikosi kazi hicho kimependekeza kuimarishwa utamaduni wa kufanya mazunguzmo na kufikia maridhiano ya shughuli za kisiasa kuimarisha uzalendo wa taifa katika kufanya shughuli za siasa, kuboresha utendaji wa baraza la vyama vya siasa, kupendekeza namna bora ya kujenga utamaduini wa kuaminiana kati ya Serikali na vyama vya siasa, wanasiasa na taasisi zingine na kuhakikisha demokrasia ndiyo mchezo pekee unaotawala nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali ichukue hatua kudhibiti mfumuko wa bei

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kufanya tathimini dhidi ya changamoto...

Habari za Siasa

Bunge lataja kinachokwamisha Mradi wa Mchuchuma na Liganga

Spread the love  MRADI wa uchimbaji chuma cha Liganga na Makaa ya...

Habari za Siasa

Chongolo aagiza watendaji wanaoonyesha mianya ya rushwa wakamatwe

Spread the love   KATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa...

Habari za Siasa

TRA iweke mfumo wa msamaha wa kodi kutekeleza miradi

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kimeitaka Mamlaka ya Mapato...

error: Content is protected !!