Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uamuzi wa mahakama: Lissu aibuka na hoja nzito
Habari za Siasa

Uamuzi wa mahakama: Lissu aibuka na hoja nzito

Tundu Lissu, Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki akiwa hospitali ya Nairobi nchini Kenya
Spread the love

Nimewasiliana na wakili Peter kibatala kuhusu uamuzi wa Jaji Matupa wa leo. Huu ndio aina ya uamuzi unaotolewa na Mahakama iliyoingiwa na hofu ya watawala na kuwa compromised. Anaripoti Mwandishi wetu

Sisi hatukuwa, na bado hatuna, ugomvi na Tume ya Uchaguzi wala na Miraji Mtaturu. Ukifungua kesi ya uchaguzi, kama anavyoshauri Jaji Matupa, unatakiwa kuthibitisha kwamba una ’cause of action’, i.e. ugomvi na aliyechaguliwa au aliyesimamia uchaguzi. 

Tume iliitisha uchaguzi kwa sababu iliandikiwa barua na Spika Ndugai kwamba kiti cha ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kiko wazi. Haijatukosea sisi na, kwa sababu hiyo, hatuwezi kuishtaki kwa njia ya kesi ya uchaguzi.

Miraji Mtaturu aligombea uchaguzi na kutangazwa ‘mshindi’ kwa sababu aliitikia wito wa Tume. Hajatukosea sisi na, kwa sababu hiyo, hatuwezi kumshtaki kwa kutumia njia ya kesi ya uchaguzi.

Aliyetukosea ni Spika Ndugai; na ‘dawa’ stahiki kwa makosa yake sio kesi ya uchaguzi, bali ni marejeo ya kimahakama ya uamuzi wake. Hatukukosea chochote kufungua maombi ya marejeo ya kimahakama.

Hoja ya kwamba kutakuwa na mgogoro wa kikatiba, wabunge wawili, etc., ni hoja isiyokuwa na mantiki au maana yoyote.

Tulichoomba sisi ni Mahakama Kuu itamke kama uamuzi wa Spika Ndugai ulikuwa sahihi kisheria. Once Mahakama Kuu ikitamka kwamba uamuzi huo haukuwa sahihi kisheria, maana yake ni kwamba yote yaliyofanywa na Tume kufuatia uamuzi huo yalikuwa batili.

Kama uamuzi wa Spika Ndugai ni batili maana yake ni kwamba uchaguzi ulikuwa batili na hakuna mbunge mpya aliyechaguliwa kihalali. Kwa hiyo hakuwezi kuwa na wabunge wawili kwenye nafasi moja.

Remedy??? Tunaenda Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Tutajua kama tuna Mahakama ya Tanzania au tuna ‘Mahakama’ ya Tanzania!!!

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!