Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Uamuzi kina Mdee: Chadema yampa zigo AG, Spika Tulia
Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi kina Mdee: Chadema yampa zigo AG, Spika Tulia

Spread the love

 

BAADA ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu kuyatupilia mbali maombi ya Halima Mdee na wenzake 18 ya kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama wa Chadema, Katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, amemuomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), awasilishe taarifa kwa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ili awaondoe bungeni. Wanaripoti Waandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mnyika ametoa maombi hayo leo Jumatan tarehe 22 Juni 2022, muda mfupi baada ya mahakama hiyo mbele ya Jaji John Mgetta, kuyatupilia mbali maombi hayo akisema yalifunguliwa kinyuke cha sheria kwa wahusika kushindwa kutaja jina sahihi la mjibu maombi.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema amesema, hakuna tena sababu za wabunge hao akiwemo Halima Mdee, kubaki bungeni kwa kuwa wamefukuzwa uanachama.

“Katika kesi hii Serikali iliwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, tunaimani atapeleka taarifa kwa Spika. Naamini kuanzia section ya Bunge inayoendelea leo atapaswa kitekeleza matakwa ya kikatiba ya kuwaondoa,” amesema Mnyika na kuongeza:

“Spika na mwanasheria wa Serikali watekeleze matakwa ya kikatiba sababu hakuna zuio la kisheria, hakuna kisingizio.”

Mbali na Mdee, wengine waliofukuzwa Chadema, ni waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu (CC), Esther Matiko na Ester Bulaya; aliyekuwa makamu mwenyekiti wa Bawacha (Bara), Hawa Subira Mwaifunga na aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega.

Wengine, ni aliyekuwa Katibu mkuu wa Baraza la Vijana la chama hicho (BAVICHA), Nusrat Hanje; aliyekuwa Naibu katibu mkuu wa Bawacha (Bara), Jesca David Kishoa; Cecilia Pareso, Agnesta Lambart, ambaye alikuwa mwenezi wa Bawacha na Tunza Malapa, aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema, mkoani Mtwara.

Katika orodha hiyo, wamo pia Asia Mohammed, aliyekuwa Naibu Katibu mkuu wa Bawacha (Zanzibar), Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Flao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!