Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya leo Ijumaa tarehe 3 Juni 2022, inatarajia kutoa uamuzi wa kupinga Askofu mteule, Geofrey Mwakihaba wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Konde asisimikwe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Kesi hiyo imefunguliwa aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Edward Mwaikali pamoja na mambo mengine anapinga Mwakihaba kusimikwa Jumapili hii tarehe 5 Juni 2022.

Jaji anayesikiliza kesi hiyo ni James Karayemaha ambaye tarehe 1 Juni 2022 alisikiliza hoja za pande zote mbili na kuiahirisha hadi leo Ijumaa.

Ni kesi namba 3/2022 na kesi namba 14/2022 ambazo ziliahirishwa tarehe 31 Mei 2022 ili kupisha majadiliano yaliyokuwa yakiendelea baina ya Serikali na pande zinazotofautinaa.

Upande wa mleta maombi Askofu Edward Mwaikali umewakilishwa na Wakili William Mashoke, Samson Mbamba na Godwin Mwapongo.

Wakili wa wajibu maombi wakiongozwa na Dk. Pallangyo aliiambia mahakama wakili Azael Mwaiteni na Benjamin Mbembela wameamua kujiondoka kwenye shauri hilo na kwamba watakuja endapo Mahakama itawahitaji.

Baada ya kujiondoa mawakili wote wawili, Mahakama iliendelea kusikiliza mashauri yote mawili kesi namba tatu ya mwaka 2022 na kesi namba 14 ya mwaka 2022.

Shauri la kwanza ambalo lililetwa na mleta maombi ni kupinga kuondolewa madarakani, kutakiwa kurejesha vitendea kazi vya uaskofu na shauri la pili kuzuia uapisho wawajibu maombi namba nne na namba tano.

Wakili Dk Pallangyo aliiambia Mahakama kuwa hoja zililetwa na mleta maombi hazina mashiko na pia Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi sababu sula hilo ni lakidini na kiimani.

Kutokana na hoja Wakili Pallangyo, aliiomba Mahakama kutupilia mbali hoja za mleta maombi sambamba na kulipa gharama za kesi.

Kwa upande wa Wakili wa mleta maombi, Samson Mbamba, ameiambia mahakama utaratibu uliotumika kufanya mkutano mkuu, 22 Machi 2022 na kumchagua mjibu maombi namba nne na tano haukuwa halali kwa mujibu wa katiba ya KKKT Dayosisi ya Konde, kifungu namba 13 ya mwaka 2015.

Akirejea baadhi ya kesi ambazo shughuli zote zilizohusu taasisi zilisitishwa wakati kesi ya msingi ikiendelea mahakamani, hivyo kutolewe zuio la kusitishwa kwa shughuli za uapisho na kukabidhi ofisi na vifaa vyote vya kiuaskofu.

Katika hoja hiyo wakili, Godwin Mwapongo aliiambia mahakama kuwa hali hiyo imeleta mkanganyiko baina ya pande zote mbili na kusababisha baadhi ya waumini kufunguliwa kesi za jinai namba 45 na 46 ya mwaka 2022 kwenye kanisa la KKKT Matema.

Wakili Mwapongo akasema zuio la uapisho litasaidia kuleta amani na kutoa nafasi kwa kesi ya msingi kusikilizwa mahakamani badala ya upande wa mjibu maombi kuendelea na shughuli za uapisho zinazotarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *