Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Twitter na Facebook, zamfungia Trump
Kimataifa

Twitter na Facebook, zamfungia Trump

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump
Spread the love
MITANDAO ya Twitter na Facebook, imezifunga kwa muda akaunti za rais wa Marekani, Donald Trump, kufuatia kutuma ujumbe kwa wafuasi wake waliovamia Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika ujumbe uliotumwa katika mitadao hiyo kwa waandamanaji hao, Rais Trump alisema, “nawapenda” na kuwataka kwenda nyumbani.

Twitter na Facebook wameeleza pia kuwa Rais Trump ametoa madai ya uongo kuhusu udanganyifu uliofayika katika uchaguzi huo.

Twitter ilisema, Rais Trump anapaswa kuondoa jumbe zake tatu alizoweka kutokana na ukiukwaji wa maadili.

Kampuni hiyo imesema, iwapo Trump atakaidi agizo la kufuta jumbe zake hizo, akaunti zake za twitter zitafungwa kabisa.

Imesema, “ukiukaji wa sheria za twitter siku zijazo utasababisha kufutiliwa mbali kwa akaunti ya @realDonaldTrump account.”

https://twitter.com/TwitterSafety/status/1346970432017031178

Hatua hiyo ina maana kwamba siku za Donald Trump katika mtandao wa twitter zinahesabika.

Rais huyo anajulikana kwa kutoheshimu masharti ya muongozo wa twitter kuhusu jamii.

Nayo kampuni ya facebook imemfunga Rais Trump kwa saa 24, na kwamba YouTube pia iliondoa video hiyo.

Facebook imesema: Tuliiondoa kwasababu tuliamini kwamba inachochea badala ya kupunguza ghasia zilizokuwa zikiendelea.

Wafuasi wake walivamia Bunge la Marekani na kukabiliana na maafisa wa polisi kitu kilichosababisha kifo cha mwanamke mmoja.

Ghasia hizo zilisitisha mjadala kuhusu ushindi wa rais mteule, Joe Biden.

Kabla ya ghasia hizo, rais Trump aliwaambia wafuasi wake mjini Washington kwamba uchaguzi huo uliibwa.

Saa chache baada ya ghasia kuzuka ndani na nje ya jumba la Capitol Hill, alionekana katika video akirejelea madai hayo ya uongo.

You tube ilisema kwamba iliiondoa kanda hiyo ya video kwasababu ilikiuka sera za kusambaza madai ya udanganyifu kuhusu uchaguzi uliopita.

Awali twitter haikuwa imeiondoa video hiyo, na badala yake kuondoa uwezo wake wa kujibiwa, kupendwa na kutolewa maoni.

Lakini baadaye iliiondoa na kufuta akunti ya rais huyo anayeondoka madarakani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!