November 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Twiga wa ATCL ‘amnogesha’ JPM, amwaga mamilioni

Spread the love

KAZI ya upakaji rangi, sambamba na uchoraji wa picha ya Twiga kwenye ndege ya viongozi wa serikali iliyotolewa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kusafirisha abiria, imempa tabasamu kiongozi huyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kutokana na furaha ya kuona kazi nzuri inayofanywa na Watanzania wazalendo kwa bei ya chini, imemsukuma Rais Magufuli kuwapa zawadi ya Sh. 10 Milioni mafundi wanaoendelea na kazi ya upakaji rangi ndege hiyo.

Rais Magufuli alikutana na mafundi wanaoendelea na kazi hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza, muda mfupi baada ya kukabidhiwa ripoti ya utendaji ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 28 Machi 2019.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Rais Magufuli alionesha kuridhishwa na kazi inayofanya na Watanzania hao ambapo aliamua kuwazawadia Sh. 10 Mil. Ndege hiyo aina ya Foker 50 iliyokuwa ikitumiwa kubeba viongozi wa nchi ambapo sasa itaanza kubeba abiria.

Kabla ya kufanya ziara hiyo, akiwa kwenye kikao chake na Takukuru, Rais Magufuli alieleza namna maofisa wa Shirika la Ndege Taznania (ATCL) walivyotaka kutekeleza ‘dili’ la upakaji na uchoraji ndege hiyo.
Alisema, maofisa hao walikuwa wamechonga mpango wa kuisafirisha ndege hiyo nje ya nchi kwa ajili ya kupakwa rangi na kuchorwa twiga kabla ya kuanza ATCL kubeba abiria.

Rais Magufuli alisema, baadaye ATCL ikashauri kuwa, kazi ya rangi na mnyama huyo (Twiga) inatakiwa ikafanywe nje ya nchi, hata hivyo hakuafiki.

“Wakasema haya maneno kuyaandika na kuchora twiga hayawezi kufanyika Tanzania, hayupo mtu wa kufanya hivi, zikatafutwa nchi tatu za nje zinazoweza kufanya hiyo kazi, sitaki kuzitaja.

“Nikasema jamani hapana, tafuteni wataalamu wenu hapahapa nchini wanaojua kuchora, watashindwa kuchora twiga kweli. Mbona wanajua kuchora simba? Wakakaa kimya wakifikiri nimesahau, wakawa wametafuta nchi fulani kimyakimya ili waipeleke hiyo ndege.” Amesema.

Na kwamba, baadaye aliambiwa “ile ndege inaondoka kesho”’ naye akawambia “na wao watakaoisindikiza hiyo ndege.” Wakati maofisa hao wakimweleza kuwa ndege inaondoka, walikuwa tayari wamelipa Dola za Marekani 28,000 (Sh. milioni 65) na malipo ya awali ya asilimia 60 yameshalipwa kule zinakopelekwa pamoja na gharama ya wahudumu wa ndege wataoisindikiza.

“Nikajiuliza ndege inakwenda gereji, sasa hawa wahudumu wanakwenda kumhudumia nani? Na siku za ukarabati zilizopangwa zilikuwa 15 hadi 30, nazo zikiwa zimelipiwa ili wakati ndege inapakwa, wawe wanaisubiri.

“Nikasema hii ndege ikiondoka, hao wote waliohusika wanaondoka saa hiyohiyo, ikiwa inapaa na wao wanaondoka.”

 

 

error: Content is protected !!