TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘’Twiga Stars’’ imeendeleza ubabe katika michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Ukanda wa Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa upande wa wanawake baada ya kushinda mechi zake zote za makundi na kutinga hatua ya nusu fainali. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).
Twiga Stars inayoshiriki michuano hiyo timu iliyoalikwa ilishuka dimbani siku ya leo Oktoba 4 kukabiliana na Timu ya Taifa ya Sudan Kusini na kuibuka na ushindi wa bao 3-0 katika dimba la Nelson Mandela Stadium, huku mabao yote yakifugwa na Stumai Athumani na kuchaguliwa kuwa nyota wa mchezo.
Timu hiyo imekua na kiwango kizuri baada ya kushinda mechi zake mbili za awali zote katika hatua ya makundi kwa kuzifunga Timu Botswana 2-0, na Zimbabwe 3-0 na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayofanyika huko Afrika Kusini.
Leave a comment