October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tweweza ladai kupokea vitisho

Aidan Eyekuze, Mkurugenzi Twaweza

Spread the love

SHIRIKA lisilo la kiserikali linalojihusisha na utafiti  la Twaweza, limedai kuwa limelazimika kufuta mkutano wake na waandishi wa habari, uliolenga kutoa tathimini ya hali ya uhuru wa kujieleza nchini, kufuatia maofisa wake kupokea vitisho kutoka serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Aidan Eyakuze, amenukuliwa akisema, shirika lake limeamua kuufuta mkutano huo, baada ya viongozi wake, kushinikizwa na baadhi ya viongozi serikalini.

Alisema, waliokuwa wakitoa vitisho waliwaambia maofisa wa Taweza kuwa ni muhimu mkutano huo ukasitishwa, kutokana na kile walichokiita, “usalama wa umma.”

Hata hivyo, Eyakuze hakuwataja maofisa wa serikali aliodai walishinikiza kufuta mkutano wake huo. Mkutano kati ya Twaweza na wanahabari, ulipangwa kufanyika tarehe 1 Novemba 2019, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Alisema, “mnamo majira ya saa 4 asubuhi ya tarehe 1 Novemba 2019,  tulipanga kufanya mkutano na waandishi wa habari, kwa ajili ya kutoa data za uchumi. Lakini kuanzia saa 1.38 asubuhi, uongozi wa Twaweza ulianza kupata shinikizo kubwa kutoka serikalini kutaka kuaghirisha mkutano huo.”

Kwa mujibu wa Eyakuze, waliokuwa wanashinikiza kutofanyika kwa mkutano huo, walikuwa wakidai kuwa hatua hiyo inalenga kulinda maslahi ya usalama wa umma.”

Twaweza – shirika linaloshughulika na masuala ya utafiti nchini Tanzania –limejipatia umaarufu mkubwa nchini katika miaka ya karibuni, kutokana na kazi zake za kitafiti, hasa katika maeneo ya elimu, uhuru wa kujieleza, uchumi na fedha.

Pamoja na mafanikio hayo, shirika hilo na baadhi ya watendaji wake, akiwamo Eyakuze, wamekuwa wakisumbuliwa na vyombo kadhaa nchini. 

Mathalani, Eyakuze mwenyewe, ametuhumiwa kutokuwa raia na kwa takribani sasa ni mwaka mmoja na nusu, hati yake ya kusafiria inashikiriwa na Idara ya Uhamiaji.

Aidha, Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), imeiandikia barua kadhaa, ikitaka taasisi hiyo kujieleza kutokana na “kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa.”

Mkutano kati ya Twaweza na waandishi wa habari ambao umefutwa ghafla, ulilenga kutoa ujumbe wake katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya waandishi wa habari ulimwenguni, yaani the International Day to End Impunity for Crimes Against Journalists.  

Kwa miaka mingi, Tanzania imekuwa katika ramani nzuri ya hasa kwenye uhuru wa kujieleza na suala la amani na uhuru wa demokrasia.

Hata hivyo, kwa miaka mitano iliyopita, katika kanda ya Afrika mashariki, ilikuwa ikiongoza katika masuala ya uhuru wa kujieleza lakini sasa taifa hilo linaangalia taifa la Kenya kama mfano.

error: Content is protected !!