December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tuzo CAF kutolewa Januari mwakani

Spread the love

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imetangaza tarehe 8 Januari, 2019 itafanyika hafla ya utoaji tuzo mbalimbali za wachezaji pamoja na timu zilizofanya vizuri katika michuano iliyoandaliwa na shirikisho hilo kwa mwaka 2018 kuanzia Febuari mpaka Novemba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Vipengele ambavyo vitawaniwa tuzo katika hafla hiyo ni pamoja na Mchezaji Bora wa Mwaka, Kocha Bora, Mchezaji Bora Chipukizi, Kocha Bora wa kike, Mchezaji Bora wa kike, Timu bora ya mwaka kwa wanaume, Timu bora ya mwaka kwa wanawake, Goli bora la mwaka, Kikosi Bora cha mwaka.

Maadhimio hayo yamekuja baada ya mkutano wa kamati kuu ya shirikisho hilo uliofanyika wiki iliyopita mjini Dakar, Senegar na kuamua kwa pamoja kuwa hafla hiyo itafanyika katika mji mji huo mapema mwakani.

error: Content is protected !!