July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tuzo BET: Elfu 19 wampinga Dimaond

Naseeb Abdul 'Diamond Platnum’

Spread the love

 

KAMPENI ya kuhakikisha msanii wa muziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ anaondolewa kwenye mbio za kuwania tuzo za Black Entertainment Television (BET) imeshika kasi. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Diamond ni msanii pekee kutoka Tanzania, anayewania tuzo hizo ambazo kilele chake kitakuwa tarehe 27 Juni 2021, nchini Marekani.

Tangu BET ilipotoa orodha ya wanaowania tuzo hizo, ikiwemo ya Diamond anayewania kipengele cha msanii bora wa kimataifa na wasanii wengine saba, wadau wa haki za binadamu nchini Tanzania, wamepinga uteuzi wake.

Wengine kwenye kipengele hicho, Diamond anachuana na; Wizkid (Nigeria), Burnaboy (Nigeria), Ayanakamura (Ufaransa), Emicida (Brazil), Headie (Marekani), Young T & Bugsey na Youssoupha wa Ufaransa.

Katika kushinikiza BET inamwengua kwenye kinyang’anyiro hicho, mtandao wa Change.org inakusanya saini za watu mbalimbali ili kushinikiza waandaaji wa tuzo hizo kumtoa.

Miongoni mwa sababu zinazoelezwa kwenye ukurasa huo wa kukusanya saini ni Daimond, kushindwa kutumia nafasi yake kutetea ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania.

Pia, sababu nyingine ni Diamond, alishindwa kukemea vikali kitendo cha msanii mwenzake, Roma Mkatoliki, Nay wa Mitego na Idris Sultan walipokuwa na kadhia za ukiukwaji wa haki za binadamu. Roma alitekwa na watu wasiojulikana, kisha kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili.

Hadi kufikia leo Jumanne, tarehe 8 Juni 2021, saa 9:25 mchana, waliokuwa wamesaini fomu hiyo ni zaidi 19,901.

Katika ukurasa huo, imewekwa picha ya msanii Diamond na aliyekuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hayati John Pombe Magufuli, wakiwa kwenye moja ya mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Picha hiyo ni, Hayati Magufuli alimvalisha kofia Diamond.

Mara baada ya kumalika kwa ukusanyaji wa saini hizo, wahusika wa mtandao huo, wanakusudia kuzifikisha BET. Ingawa bado haijafahamika kama zitachukuliwa kwa uzito na kuondolewa.

error: Content is protected !!