January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tutavuna wabunge 5, madiwani 16 CCM

Viongozi wa Chadema wakiwa katika moja ya maandamano yao

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Morogoro, kimejinasibu kuwa kwa jinsi upepo wa kisiasa unavyokiendea kombo kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), watanyakua wabunge watano na madiwani 16 watakaochoshwa na rushwa wakati wa kura za maoni. Anaandika Bryceson Mathias, Morogoro… (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISIOnline, Katibu wa Chadema Morogoro, Samwel Kitwika, amesema, rushwa, ukiritimba na mchezo mchafu uanaoendelea ndani ya CCM kuwapata wawakilishi hao, ndio mtaji na mvuto utakaowakimbiza.

Alipoulizwa iwapo anaweza kuwataja wanasiasa hao, Kitwika amesema, ”Kwa sasa hatuwezi kuwataja wabunge na madiwani hao, maana ni sawa na kumuonesha adui mbinu zako, isipokuwa ifahamike wanatoka katika majimbo yote 10 ya mkoa na kata zake.

“Sababu kubwa inayotangulia katika kufikia maamuzi hayo ni umaarufu wa Chadema tangu ngazi ya taifa hadi msingi, vikiunganishwa na uadilifu na umoja ndani ya chama.

Kitwika ameongeza kwamba, awali walikuwa na madiwani 10 waliofika kwenye ofisi za Chadema kuomba kuungana na chama kulileta ukombozi wa kweli kwa wananchi walioumizwa na rushwa na maovu, lakini wiki hii wameongezeka wengine sita.

error: Content is protected !!