July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tutashinda uchaguzi, tukiwa wamoja – Mnyika

John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka viongozi na wanachama wake kuanza mikakati ya chini kwa chini, ili kumsaidia Tundu Lissu, aliyepitishwa na chama hicho, kuwania urais katika uchaguzi ujao,  kushinda uchaguzi huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza …(endelea).

Akizungumza katika uzinduzi wa Sera ya Baraza la Vijana la chama hicho (Bavicha), jijini Mwanza, mwishoni mwa wiki iliyopita, katibu mkuu wa chama hicho, John Mnyika amesema, ili Lissu aweze kushinda uchaguzi huo, ni sharti kufanyike kazi.

Uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, umepangwa kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu, na Mnyika anasema, ili Chadema na Lissu wake, weweze kuingia Ikulu, ni lazima wanachama wa chama hicho, waanze kutekeleza mikakati ya ushindi.

Tayari Lissu na mgombea wake mwenza Salum Mwalimu, wamechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Wote tunataka Tundu awe rais, Chadema iingie Ikulu. Lakini ili hilo litimie, ni lazima na kuanzia leo, kama wewe ni bodaboda au mama lishe, kabla kampeni kuanza, mikakati ya chini chini imeanza, inatakiwa na sisi tuanze.

“Wewe sema mimi nitahakikisha hizi kura za eneo lote ni mtaji wangu nitauona C hadema, unaanza maandalizi mapema ili tukifika hatua ya pili ya mashambulizi, tunafanya kampeni kidogo tunamaliza kazi.”

Kwa mujibu wa ratiba ya NEC, kampeni zitafunguliwa rasmi tarehe 26 Agosti 2020 na kufika tamati tarehe 27 Oktoba mwaka huu.

Aidha, Mnyika amewataka wanachama wa Chadema kushikamana ili kuhakikisha wagombea wake katika uchaguzi huo wanashinda.

“Jambo lingine ambalo hatupaswi kubishana ni nguvu ya imani katika vita, hili nalo hatupaswi kubishana sababu msingi wake ni wa kikatiba. Nawaomba niwaambie uchaguzi ni vita, vita hii ni ya kidemokrasia na silaha yake ni kupiga kura na si bunduki,” ameeleza Mnyika.

Chadema kilimpitisha Lissu kuwa mgombea wake wa urais, katika mkutano wake mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaa, mwanzoni mwa mwaka huu.

error: Content is protected !!