August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tutaendelea kuhoji – Jussa

Spread the love

 

KAIMU Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ismail Jussa Ladhu amesema mjadala kuhusu kasoro za kiutendaji katika utekelezaji miradi ya maendeleo hautasimama mpaka pale kutapotolewa maelezo ya kutosheleza. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Jussa ambaye anakaimu nafasi ya Zitto Zuberi Kabwe aliyeko safarini nje ya nchi, amesema ni msimamo wa chama chake kuwa bado yapo mambo ya msingi hayajajibika pamoja na maelezo mengi yaliyotolewa hivi karibu na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Ofisi Kuu ya Chama, Vuga mjini hapa, Jussa amesema suala muhimu linalohitaji maelezo ya kutosheleza ni kueleza mambo kwa uwazi ikiwemo sababu za usimamizi wa utoaji wa miradi na ukodishaji visiwa visivyoishi watu kutofanywa na Bodi za mamlaka husika za kiserikali.

Amesema badala ya Bodi za mamlaka husika ikiwemo Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (ZAA), kushughulikia utaratibu wa kutafuta watoa huduma, jukumu hilo linasimamiwa na kiitwacho Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT).

Jussa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu wa ACT Wazalendo, amesema utaratibu wa kutumia timu una maana sheria ya manunuzi ya umma ya Zanzibar imevunjwa.

Amesema kwa mfano sheria hiyo Nam 11 iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, inapaswa kutumika kwa fedha zote hata zile mkopo akisisitiza “mkopo wa serikali hulipwa kwa kutumia fedha za wananchi kupitia kodi zao.”

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Amehoji haya kwa nguvu ya wajibu wanaopewa wananchi wa Zanzibar na Katiba yao kulinda mali ya umma na kusimamia mwenendo wa serikali.

Jussa amerudia kuhoji kiwango cha uzingatiaji wa sheria, taratibu na kanuni za utendaji wa serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo tangu ishike mamlaka serikali inayoongozwa na Dk. Mwinyi; na ameeleza wazi kuwepo harufu ya ufisadi kwa baadhi ya miradi na vile wawekezaji na au wakandarasi walivyopewa kazi.

Jussa amesema anajua ACT Wazalendo ni sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, lakini bado chama kinao wajibu wa kutekeleza kwa kuwa kinahakikisha kuna uwajibikaji wa kutosha serikalini.

“Wenzetu walioko Serikalini na Baraza la Wawakilishi wana wajibu wao kikatiba kama tulivyonao sie tuliobaki kwenye chama. Tunatekeleza wajibu wetu kwa mamlaka ya kikatiba,” alisema.

Aliulizwa iwapo anachokifanya kitaeleweka kwa wananchi wanaojua kuwa chama hicho ni sehemu ya serikali iliopo sasa.

error: Content is protected !!