Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa “Tusiiogope sheria ya vyama vya siasa tuikabili”
Habari za Siasa

“Tusiiogope sheria ya vyama vya siasa tuikabili”

Spread the love

NI siku ya tatu tangu Serikali kuifikisha Bungeni Muswada wa sheria ya vyama vya siasa nchini ambapo umoja wa vyama vya siasa visivyokuwa na wawakilishi bungeni vimetoa wito kwa wanasiasa wengine wasiiogope muswada huo bali waupitie ili kuuboresha. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Vyama hivyo ni pamaja na chama cha DP NRA, chama cha Wakulima AFP, Chama cha Wafanyakazi TLP, Chama cha Sauti ya Umma (Sau) UMD, UDP, na Demokrasia Makini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Abdul Mluya Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia cha DP amesema kuwa wanasiasa waache kupotosha kuhusua muswada huo ambao siyo mgeni kwa vyama vyote vya upinzani.

“Muswada huu tulifikishiwa sisi wapinzania tangu mwaka 2013 tukaujadili na mapendekezo yetu yamezingatiwa ingawa huu muswada hatujapatiwa lakini tunamuomba msajili wa kwa vile muswada huo ni sehemu ya Umma sasa atuletee tuujadili,” amesema Mluya.

Amesema kuwa yale ambayo yalikuwemo kwenye maoni yao yale ambayo yatavisaidia kutetea maslahi ya vyama vya kisiasa.

Ametosa mfano wa adhabu ya chama cha siasa kikikosea kwa sheria iliyokuwepo sasa kinafutwa lakini kwenye maoni yao ambayo anaimani yamefanyiwa kazi kwenye nuswada huo vyama vya siasa vikikosea vitaonywa au faini ikibidi ndio vifutwe .

Rashid Rai Katibu Mkuu wa chama cha Wakulima AFP amesema kuwa sheria ni mzuri kwa watu ambao ni waadilifu na wale wasio kuwa waadilifu hugopa sheria kwa sababu ya kuhofia kuhukumiwa.

Amesema kuwa viongozi na wafuasi wa vyama vya siasa wasiogope muswada huo ambapo zipo sheria zenye kuwajkamata wabadhirifu na zipo sheria zenye kutetea maslahi ya vyama vya siasa.

Saum Rashid Katibu Mkuu wa chama cha UDP amesema kuwa muswada huo sio mgeni kwa vyama hivyo ambapo ameiomba serikali kuvipa nafasi vyama vya siasa kuujadili muswada huo.

Agostino Mrema Mwenyekiti wa chama cha TLP amemtaka Rais John Magufuli kuvisaidia vyama vidogo visivyokuwa na wawakilishi navyo vipate nafasi kwenye bunge .

Amesema kuwa rais akivisaidia vyama hivyo ataacha alama kwenye tawala yake na atakumbukwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!