January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tunzo ya mwanamke jasiri duniani

Rais wa Tanzania Women Archievement (TWA), Irene Kiwia akizungumza na waandishi wa habari hawamo pichani

Spread the love

TAASISI  ya Shirika la kijamii Tanzania Women of Achievement (TWA)  wamezindua rasmi Tuzo za Wanawake wenye MafanikioTanzania ambazo zitafanyika Machi 7, 2015 kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa shirika hilo, Irene Kiwia, alisema kuwa tunzo hizo pia zitaenda sambamba na mafunzo ya kujenga uwezo wa wasichana kuwa viongozi bora katika nyanja tofauti katika jamii.

Kiwia alisema wasichana hao watateuliwa kwa vigezo mbalimbali kutokana na viti tofauti walivyoonyesha katika jamii zao katika kusaidia jamii, na hata mara baada ya kupewa mafunzo hayo watakaporudi watakuwa chachu ya maendeleo katika mikoa yao.

Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatahusisha wasichana walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 27, ambayo yatachukua wiki 6 na baada ya hapo watakutanishwa na wanawake wanaofanya vizuri katika biashara na kazi zingine za kijamii kwa jili ya kuwapa hamasa.

Pia Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Sadaka Gandhi alisema tunzo ya mwaka huu zimegawanyika katika nyanja mbalimbali kama sanaa, utamaduni, ujasiliamali, elimu afya, kilimo na michezo, ambapo wasichana watakaoshiriki watatoka mikoa mbalimbali.

“Tunaomba katika miezi hii mitatu, watu wajitokeze kuchagua wanawake ambao wanafanya vizuri katika jamii zao, na kuleta mabadiliko katika mkoa wake, unaweza kumpendekeza au yeye mwenyewe akajipendekeza kupitia namba zetu 0658 870116,” alisema Sadaka.

Gandhi alisema shirika hilo waliloliazisha mwaka 2009 likiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia maendeleo Tanzania katika nyanja tofauti.

Habari hii imeandikwa na Sarafina Lidwino

 

error: Content is protected !!