Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Tunduma waiangukia Serikali kukamilisha ujenzi sekondari ya Samia
Elimu

Tunduma waiangukia Serikali kukamilisha ujenzi sekondari ya Samia

Spread the love

WADAU wa elimu mkoani Songwe wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa mabweni katika shule mpya ya wasichana ya Dk. Samia S.H sekondari inayojengwa kwa ili wanafunzi waanze kulala hapo kutokomeza mimba za utotoni. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Shule hiyo inayojengwa kwa gharama ya Sh tano bilioni ipo mtaa wa Namole kata ya Chiwezi katika mji wa Tunduma imesajiliwa kwa namba S.6238 mwaka 2023 ikitarajia kupokea wanafunzi 251 kuanza mwezi Agosti 2023.

Wakizungumza na MwanaHalisi Online baadhi ya wakazi hao wa Tunduma, Salama Nakamwela amesema shule hiyo inayojengwa kwa ubora ipo pembezoni mwa mji, itakuwa mkombozi kwa watoto wa kike hivyo anaiomba serikali kuharakisha ujenzi huo hasa mabweni kabla ya agosti.

Isakwisa Mwampashi mkazi wa Mbozi naye aliunga mkono uharaka huo na kusisitiza kuwa shule hiyo itakuwa muarobaini kwa watoto wa kike kukatishwa masomo kutokana na ujauzito.

Amesema vitendo vya wanafunzi kwenda shule na kurudi wanakumbana na vishawishi hivyo mabweni yaharakishwe.

Kaimu afisa elimu sekondari wa halmashauri, Christina Mwita amesema maombi ya wananchi yana mashiko kwani tayari ujenzi upo asilimia 70 ila majengo muhimu kama utawala, madarasa 10 ya ghorofa, matundu 24 ya vyoo, mabweni na ofisi nne za walimu zipo hatua za umaliziaji huku wakihitaji walimu 32.

Amesema wanaendelea kuharakisha miundombinu mingine ikiwemo maji, umeme pamoja na samani za ofisi na vitanda vya dabo deka 120 sawa na vitanda 240  ambavyo tayari vimeanza kukamilishwa ikiwemo bajeti ya chakula.

Amesema mradi huo unajengwa kwa Sh tano bilioni ambapo serikali kuu ilitoa Sh nne bilioni na Sh moja bilioni imetolewa na halmashauri kupitia mapato yake ya ndani.

Mkuu wa mkoa wa Songwe, Dk.Fransis Michael amewapongeza watumishi wa halmashauri ya  mji Tunduma kwa usimamizi mzuri wa ujenzi huo huku akiungana na wananchi kutaka ukamilike haraka hasa majengo muhimu wanafunzi waanze kusoma.

Hatua ya wananchi hao kuomba ujenzi uharakishwe ulikuja baada ya kamati ya siasa ya CCM mkoa chini ya mwenyekiti wake Ladwel Mwampashi kufika na kukagua utekelezaji wa ujenzi wa shule hiyo huku wakipongeza ubora wa mradi na kutaka ujenzi uharakishwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!