April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tundu Lissu ‘kujinoa’ Marekani, Ulaya

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema

Spread the love

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekwenda Marekani na baadaye Ulaya. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Nchini Marekani, Lissu anatarajia kufanya mazungumzo na viongozi wa Serikali ya Washington.

Kwa mujibu wa taarifa yake aliyoitoa leo tarehe 3 Oktoba 2019, mwanasiasa huyo atazungumza na viongozi wa Marekani katika ziara ya siku 11 nchini humo na Ulaya.

Pia, Lissu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Mashariki, atafanya mazungumzo na wabunge, taasisi za kimataifa na sekta binafsi za nchini Marekani.

“Kwenye ziara ya Marekani nitakutana na viongozi wa Serikali, wabunge wa Marekani, taasisi za kimataifa na sekta binafsi, vyombo vya habari, pamoja na Watanzania waishio Marekani,” inaeleza taarifa ya Lissu.

Lissu ameanza, ziara nchini Marekani jana tarehe 2 Oktoba 2019 na anatarajia kumaliza tarehe 13 Oktoba 2019.

“Jana Oktoba 2, 2019 nimeanza ziara nchini Marekani, itakayonichukua hadi tarehe 13 ya mwezi huu. Niko Atlanta, Georgia, hadi tarehe 6. Kati ya tarehe 7 na 9 nitakuwa Washington DC, na kati ya tarehe 10 na 12 nitakuwa Houston, Texas,” inaeleza taarifa ya Lissu.

Baada ya ziara yake nchini Marekani, Lissu ataendelea na ziara yake barani Ulaya, ambapo tarehe 15 hadi 20 Oktoba, 2019 atakwenda nchini Ujerumani.

Aidha, Lissu amezungumzia rufaa ya kesi yake kuhusu kupinga kuvuliwa ubunge wa Singida Mashariki, akisema kwamba amekamlisha taratibu zote.

“Kuhusu rufaa ya kesi yangu, hiyo ni kwamba tumekamilisha taratibu zote za mwanzo. Kilichobaki ni kupata mwenendo wa shauri lililokuwa Mahakama Kuu ili tuweze kuwasilisha rufaa yenyewe,” amesema Lissu

Kuhusu maendeleo ya afya yake, Lissu amesema “Kuhusu afya yangu, juzi tarehe 1 nilikutana na madaktari wangu na kufanyiwa vipimo vya mwisho.

“Natakiwa nikutane nao mara kwa mwisho tarehe 8 ijayo, lakini itabidi tuisogeze mbele kwa sababu ya ziara hii. Hata hivyo, tiba imeshakamilika. Kilichobaki ni kupata maelekezo ya mwisho.”

Awali, Lissu alianza ziara katika mataifa hayo tarehe 28 Januari 2019 ambapo alifanya mhadhara wa kitaaluma na pia mahojiano na vyombo vya habari.

error: Content is protected !!