December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tundu Lissu atinga kwa Obama

Spread the love
MWANASHERIA mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amewasili jijini Washington, nchini Marekani ili kuzungumza katika mdahalo wa aina yake katika chuo kikuu cha George Washington. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika ziara hiyo, Lissu ameongoza na mkewe, Alicia Magabe.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mwanasiasa huyo na chama chake jijini Dar es Salaam zinasema, Lissu atashiriki katika mjadala wa moja kwa moja unaozungumzia, “Tanzania’s Democratic Challenge,” utakaofanyika kwenye chuo kikuu cha George Washington.

Aidha, katika ziara hiyo, Lissu atapata nafasi ya kushiriki mjadala utakaongozwa na  Jenniffer Cooke, mkurugenzi wa taasisi ya Instute for African Studies (IAfS). Lissu atakuwa mgeni mwalikwa.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, katika ziara hiyo, Lissu anatarajiwa kukutana na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama. 

Lissu ambaye yuko nchini Ubelgiji kwa matibabu yanayotokana na kushambuliwa kwa risasi, yuko kwenye ziara ya nchi kadhaa za Ulaya na Marekani, kueleza kile anachokiita, “kinachoendelea nchini kuhusu demokrasia na utawala wa sheria.”

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, alishambuliwa na watu “wasiojulikana” akiwa ndani ya gari lake, alipokuwa akirejea nyumbani kwake kutokea bungeni, eneo la Area D, mjini Dodoma.

Tukio hilo lililotokea tarehe 7 Septemba mwaka 2017.

Kabla ya kupelekwa Ubelgiji, Lissu alipata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma na baadaye Nairobi nchini Kenya.

Mpaka sasa, hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kutokana na shambulio hilo.

error: Content is protected !!