August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tundu Lissu aibwaga serikali, apata dhamana

Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida (katikati), akiinga ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu

Spread the love

TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, hatimaye amepata dhamana baada ya ombi la mawakili wa serikali la kuomba mahakam imnyime dhamana kutupiliwa mbali, anaandika Hellen Sisya.

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri amesema, baada ya kupitia hoja za serikali na majibu ya mawakili wa utetezi, haoni mantiki ya kuzuia dhamana kwa Lissu.

Hivyo, Hakimu Mashauri amemtaka Lissu kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambapo kila mmoja atasaini bondi ya Sh. 10 milioni.

Lissu ametimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana, lakini anatakiwa kupewa kibali cha mahakama kila anapotaka kutoka nje ya Dar es Salaam.

Kesi itasikilizwa Agosti 24, 2017 na upande wa serikali imesema upepelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Baada ya kuachiwa Lissu na mawakili wake wamezuiwa kuzungumza nje ya mahakama.

error: Content is protected !!