July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tunazo nyumba za kibalozi 97-Kairuki

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellah Kairuki akijibu maswali bungeni

Spread the love

TANZANIA imesema inayo majengo 97 ya kibalozi katika nchi mbalimbali duniani. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angellah Kairuki amesema hayo bungeni leo, alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohammed (CUF) kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mbunge huyo alitaka kujua Tanzania inamiliki majengo mangapi kupitia balozi zake nje ya nchi na kutaka kufahamu kama serikali imepata hati miliki.

Akijibu swali hilo, Kairuki alisema kati ya majengo hayo, 88 yana hati na 9 hayana hati.

Kwamba majengo 88 yenye hati yapo katika balozi za London (8), Harare (8), Nairobi (2), Kigali (1), Kinshasa (3), Lusaka (11), Maputo (3), Tokyo (2), Roma (1), Lilongwe (5), Kampala (4), Ottawa (5), Berlin (1), Pretoria (7), Geneva (1), Bujumbura (3), Cairo (4), Washington (6), New York (4), Stockhom (3), Brussels (2), Addis Ababa (2) na Paris (2).

“Wizara yangu inaendelea kushirikiana na Balozi zetu kufuatilia upatikanaji wa hati kwa majengo ambayo hayana hati,” amesema na kuongeza kuwa:

“Waheshimiwa wabunge katika utoaji wa hati inategemeana na sheria za nchi husika na pia makubaliano kati ya nchi na nchi.”

error: Content is protected !!