June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tunajitaji rais bora, siyo bora rais

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Damian Lubuva

Spread the love

UCHAGUZI mkuu wa rais, wabunge na madiwani unakaribia kufanyika. Lakini jambo moja ni muhimu:

Taifa linahitaji rais atakayejenga nidhamu miongoni mwa raia. rais mwenye uwezo na uthubutu wa kuwaunganisha wananchi pamoja wenye itikadi na imani tofauti za kidini.

Rais mwenye uwezo wa kupambana na rushwa; ubaguzi wa kiitikadi; kidini na kulieleza taifa kuwa bila kuwa na maadili, tusitegemee miujiza.

Tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alipong’atuka na kutuachia misingi imara ya utaifa, hatujapata kiongozi wa wa kusimamia miiko; maadili na utaifa.

Tunahitaji kiongozi asiye mwathirika wa gojwa la kupendwa na mataifa ya nje kwa gharama za raia wake.

Tunataka kiongozi atakayekuwa rafiki wa vyombo vya habari na kujenga mazingira ya kukosolewa na hata kuchukiwa ili wananchi wabaini upeo wa rais wao na kule anakowapeleka!

Anahitajika kiongozi mwenye kujiamini; atakayeweza kujiuliza na kupata majibu sahihi kwa swali  maswali mazito na asiyeabudu fikra kutoka mataifa ya Magharibi.

Anahitajika rais mwenye njozi pevu, ubunifu na uadilifu. Rais mwenye dhamira safi. Rais anayeutafuta ukweli kwa bidii na kuishi kulingana na ukweli huo; na ambaye yuko tayari kulipa gharama ya kuutetea ukweli huo.

Je, yuko wapi mwanasiasa wa aina – miongoni mwa maelfu ya wanachama na viongozi wa wanaoripotiwa kusaka urais, kupitia chama tawala?

Miongoni mwa wanaotajwa kusaka urais au kujitaja, ni pamoja na William Ngeleja; January Makamba; Bernard Membe; Edward Lowassa; Steven Wassira; Mizengo Pinda;  Shamsi Nahodha; Dk. Mohammed Gharib Bilalli; Samwel Sitta; Dk. Ali Mohammed Shein; Asha Rose Migiro; Anna Tibaijuka; Anne Makinda; Prof. Juma Kapuya na Balozi Khamis Kagasheki.

error: Content is protected !!