Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tunafuatilia miradi hatufanyi mikutano ya hadhara:CCM
Habari za Siasa

Tunafuatilia miradi hatufanyi mikutano ya hadhara:CCM

Bendi ya TOT ikiwa jukwaani katika moja ya mikutano ya CCM
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekanusha madai ya kwamba chenyewe kinafanya mikutano ya hadhara huku vyama vya upinzani vikizuiwa, kikisema mkutano inayofanya na wananchi ni ya kufuatilia utekelekezaji wa Ilani yake ya uchaguzi na miradi ya maendeleo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 5 Julai 2022 na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka, alipotembelea ofisi za magazeti ya MwanaHALISI na Raia Mwema.

Ni baada ya kuulizwa iwapo chama chake CCM kinaridhishwa na hali ya vyama vya siasa vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara wakati chenyewe kikifanya kwa ajili ya kuimarisha uhai wake.

Akijibu swali hilo Shaka amesema “ni kweli CCM kinafanya mikutano lakini siyo ya hadhara, wote tunafahamu mikutano ya hadhara tafsiri yake ni nini. Kama nilivyosema CCM kimeunda Serikali na wakati tumeunda Serikali kuna mkataba na makubaliano na Watanzania tuliokwenda kuwaomba ridhaa tukawaambia ndani ya miaka mitano mkituchagua tutawaletea maendeleo.”

“Jukumu la kwanza ni kuleta maendeleo linalofanywa vizuri na Rais Samia na la pili kufuatilia yaliyoelekezwa na Serikali. Kwenye jukumu la ufuatiliaji CCM kina utaratibu mzuri wa kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa Ilani,” amesema Shaka.

Aidha, Shaka amesema CCM kina mikutano yake kuanzia ngazi ya shina hadi Halmashauri Kuu ya Taifa, ambayo inafanya kazi ya kutathimini utekelezaji wa ilani hiyo.

Mwanasiasa huyo amesema, tathimini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na ujenzi wa miradi ya maendeleo, haiwezi kufanyika pasina kuwaona na kuzungumza na wananchi wa eneo husika.

“Huwezi kutathimini bila kuwaona wananchi, lakini kuna matumizi ya fedha ya miradi ya Serikali. Nawahakikishia sio kwamba tunafanya mikutano ya hadhara, kipindi hiki tunafanya mikutano inayojipambanua moja kwa moja kwenye eneo husika yenye nasaba na lengo mahususi linalokusudiwa,” amesema Shaka.

Hata hivyo, Shaka amesema Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan, kinaendelea kufanya ya kazi ya kuangalia namna gani vyama vya siasa vitatekeleza mikutano ya hadhara.

1 Comment

  • Zungukeni Dunia nzima…
    Hakuna hata nchi moja Chama kinazunguka kuangalia miradi….hii ni kazi ya wabunge na madiwani.
    Miradi ya maendeleo ni sehemu ya uchumi wa taifa…tusiingize siasa kwenye elimu, afya , viwanda na ulinzi…eti ni sera zetu.
    CHADEMA, ACT-WAZALENDO na nyinyi muige mzunguke kukagua miradi ya maendeleo!
    Katika siasa kodi, mambo ya nje, mimba za utotoni, usharikina, mazingira, na mengineyo ndiyo mambo ya siasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

error: Content is protected !!