May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tume yaundwa kuchunguza ajali ya 5 ya moto Karume

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Ng’wilabuzu Ludigija ameunda timu ya uchunguzi wa chanzo cha moto katika Soko la wafanyabiashara wadogo la Karume ambayo inatarajia kutoa majibu kesho kuhusu chanzo cha ajali hiyo. Anaripoti Helena Mkonyi – TUDARCO … (endelea)

Soko hilo lililopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam limeungua kwa mara ya tano alfajiri ya leo tarehe 16 Januari, 2022.

Akizungumza na MWANAHALISI ONLINE, Ludigija amesema timu hiyo itajumuisha Jeshi la Zimamoto, Tanesco, Ofisi ya Mkurugenzi, Ofisi ya mkuu wa mkoa, ofisi yangu na Jeshi la polisi ili kujua chanzo cha moto.

Amewaomba wafanyabiashara kuwa watulivu wakati hatua mbalimbali zinachukuliwa na serikali kufahamu chanzo cha moto huo pamoja na hatua nyingine.

Aidha, akielezea ajali hiyo ya moto, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, John Masunga amesema baada ya kupata taarifa saa 10 alfajiri walifika eneo la tukio na kukuta moto mkubwa ambao ulisababishwa na msongamano mkubwa wa vibanda vya wafanyabiashara na bidhaa zao.

Amesema kwa kuwa vibanda hivyo vimejengwa kwa mbao imekuwa rahisi kushika moto lakini pia kilichowapa changamoto ni njia za kuelekea katikati ya soko kwa sababu soko hilo lina msongamano mkubwa wa vibanda.

“Soko la Karume si mara kwanza, ni ya nne au ya tano, mule ndani vyanzo vya moto ni vingi, kwa mfano mara ya mwisho ilikuwa ni mama ntilie aliacha majiko ya mkaa likiwa linawaka,” amesema.

Aidha, amesema hadi sasa chanzo hakijajulikana hivyo hawezi kusema ni hujuma au lah!.

Kufuatia mkasa huo, Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango wametuma salamu za pole kwa wafanyabiashara hao kutokana na hasara kubwa inayotokana na kuungua kwa soko hilo.

Aiidha, Msemaji wa wafanyabiashara ndogo ndogo ndani ya mkoa wa Dar es Salaam, Masoud Issa, amewasihi wafanyabiashara wote ambao wamepata madhara katika eneo hilo wawe watulivu wakisubiri uamuzi wa Serikali na namna watakavyosaidiwa kupata maeneo mengine ya kuendelea na biashara zao kwa sasa wakati ukarabati utakapokua unafanyika.

“Haya ndio maeneo yetu ambayo tunatafutia riziki hivyo tunaishauri serikali watujengee mfumo ambao hata zimamoto inaweza kuingia na kufanya kazi kwa haraka.

“Pia ninawaomba wafanyabiashara tuwe watulivu ili tuisikilize serikali ikifanya kazi yake na siis viongozi tuko nayo karibu,” amesema Masoud.

error: Content is protected !!