November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tume ya Uchaguzi yatangaza uchaguzi Jimbo la Nassari

Spread the love

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. Anaripoti Hamisi Mguta … (endelea).

Akitoa taarifa hiyo Jaji Kaijage amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika tarehe 19, Mei 2019 na fomu za wagombea zitatolewa kati ya Aprili 15 au 19 na uteuzi wa wagombea utafanyika Aprili 19 mwaka huu.

“Kwa kuzingatia masharti ya vifungu vya 37 na 46 vya Sheria ya Uchaguzi tume inautaarifu Umma kuhusu ratiba ya uchaguzi wa jimbo hilo, kampeni za uchaguzi zitafanyika kati ya Aprili 29 hadi Mei 18, 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni Mei 19”

Taarifa hii ya kufanyika kwa uchaguzi wa Jimbo la Arumeru inatokana na Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kukubaliana na uamuzi wa Spika Ndugai kutangaza kuwa Joshua Nassari amepoteza sifa za kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.

Nassari alivuliwa ubunge na Spika Ndugai Machi 14, 2019 kwa kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo bila taarifa rasmi.

error: Content is protected !!