Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Tume ya haki za binadamu Afrika kufanya ziara Tanzania
Habari Mchanganyiko

Tume ya haki za binadamu Afrika kufanya ziara Tanzania

Spread the love

 

TUME ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR), inafanya ziara Tanzania kuanzia tarehe 23 hadi 27 Januari 2023 kwa ajili ya kuchochoea hali ya haki za binadamu nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi karibuni na ACHPR, ziara hiyo inafuatia mwaliko uliotolewa na Serikali ya Tanzania.

Taarifa imesema ziara hiyo itakayoongozwa na Kamishna wa ACHPR Tanzania, Geereesha Topsy-Soono, ina madhumuni saba ikiwemo kuiimarisha tume hiyo pamoja na taasisi za kikanda, kwa kushirikiana uzoefu na Serikali ya Tanzania, kwa lengo la kuimarisha haki za binadamu.

“Ziara inalenga kutetea uidhinishaji wa vyombo vya kisheria vya kikanda na kimataifa vya haki za binadamu ambavyo havijiridhiwa na Tanzania,kukuza uelewa wa shughuli za tume, hasa kwa idara husika za Serikali na asasi za kiraia,” imesema taarifa hiyo.

Madhumuni mengine ni kuihimiza Serikali ya Tanzania kuwasilisha ripoti za vipindi na kushiriki mara kwa mara katika shughuli za ACHPR.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

error: Content is protected !!