April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tume Huru: Wazee Chadema ‘tatizo si Magufuli, ni Kikwete’

Hashim Juma, Mwenyekiti wa BAZECHA

Spread the love

BAZARA la Wazee la Chama cha Chadema (BAZECHA), limesema mkwamo Tume wa Huru ya Uchaguzi, umesababishwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 13 Januari 2020, jijini Dar es Salaam, Hashim Juma, Mwenyekiti wa BAZECHA amesema, Rais Kikwete anastahili lawama kutokana na kupuuza Rasimu ya Katiba ya Jaji Mstaafu, Joseph Warioba, iliyopendekeza uundwaji wa tume hiyo.

Amedai, baada ya Rais Kilwete kugundua Katiba hiyo imeweka vipengele vinavyombana rais, alimshauri Rais Magufuli kuachana na mchalato huo, ili rasimu hiyo isifanyiwe kazi.

“Tusimlaumu sana, kweli ana makosa yake lakini wa kumlaumu Kikwete (Rais Kikwete) sababu tume iliundwa, ikatumiwa mabilioni lakini mwisho wa siku alivyoona, tume inataka kuleta Tume Huru ya Uchaguzi na rais kupingwa, akaipiga chini.

“…na wakamuelekeza Magufuli (Rais Magufuli) kuipuuza Katiba Mpya. Wakati anaingia madarakani alisema, ataiendeleza baada ya kuingia madarakani akageuka akasema sio kipaumbele chake,” amesema.

error: Content is protected !!