September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tumbaku, pombe vinachochea kisukari

Spread the love

UTUMIAJI wa Tumbaku, kutofanya mazoezi, unywaji wa pombe kupita kiasi, ulaji wa lishe isiyo asilia imeelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ugonjwa wa kisukari nchini, anaandika Happyness Lidwino.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Ayoub Magimba, Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba amesema, hali hiyo inasababishwa na wananchi kutokuwa na elimu ya kujua bidhaa wanazotumia kama zinaweza kuleta ugonjwa huo.

Magimba amesema, magonjwa yasiyoambukiza yalikuwa hayapewi kipaumbele kwa muda mrefu ila mwaka 2008 kilianzishwa kitengo maalumu cha kutibu magonjwa yasiyoambukiza.

Amesema, mkakati uliopo mwaka huu 2016 hadi 2020 ni kuwa, wamepanga kuchunguza na kupima afya ya magonjwa yasiyoambukiza, upatikanaji wa dawa za magonjwa yasiyoambukiza katika vituo vyote vya kutolea huduma.

Lakini pia kuwaangalia watawafanyia nini wagonjwa watakaokutwa na ugonjwa pamoja na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu ugonjwa huo.

“Tanzania ni nchi ya kwanza katika Afrika Mashariki inayoweza kutekeleza na kufanya tafiti ya kuangalia viashiria vya ugonjwa wa kisukari ambapo tafiti zinaonesha asilimia 9.1 ya Watanzania wanakisukari, na asilimia 29 wanapresha,” amesema.

Dk. Kaushik Ramaiya, Katibu wa Kitengo cha Watafiti wa Ugonjwa wa Kisukari Afrika Mashariki ( EADSG) amesema, umuhimu na mbinu ya taifa dhidi ya vita ya ugonjwa wa kisukari ni nyenzo muhimu kwa taifa.

error: Content is protected !!