May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Tulizeni akili, mtanunua makaburi Dodoma’

Spread the love

JOSEPH Mafuru, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, amewataka wananchi wanaokwenda kununua ardhi jijini humo kutuliza akili, vinginevyo watanunua sehemu zilizotengwa kwa ajili ya makaburi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Amesema, ni lazima kwa wale wanaotaka kununua ardhi jijini humo, kufuata taratibu ili kuepuka hasara wanayoweza kupata mbele ya safari.

Mafuru ametoa kauli hiyo wakati wa kikao kilichowakutanisha wakuu wa taasisi za kiserikali za jiji hilo ambapo Dk. Binilith Mahenge, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alikuwa akipokea taarifa ya mipango ya upelekaji huduma kwenye maeneo ya uwekezaji na yanayojengwa kwa kasi jijini humo.

Amesema, hivi sasa kuna wimbi la watu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha kuvamia maporini na kununua ardhi ambayo haijapimwa.

Mafuru amesema, Jiji la Dodoma lina ramani ambayo imeeleza kila eneo na shughuli zake na kwamba, kwenda kununua bila kufuata ramani kunaweza kusababiha hasara kwa mnunuzi.

“Acheni kukurupuka” amesema Mafuru na kuongeza “mtajikuta mnanunua makaburi” na kwamba, kuna wataalamu walikuwa wakizungumza kuwa wamenunua eneo wakati eneo hilo ni chanzo cha maji Makutupora, “hiyo imekula kwao.”

Mkurugrnzi huo ameshauri kuwa, ni vizuri watu kabla ya kufanya uamuzi wowote, waulize kwenye mamlaka husika uataratibu na wataelekezwa.

“Mpango (mpango mji) mipango miji tuliyonayo ni ya miaka 20, ndiyo kwanza tupo mwaka wa kwanza,” amesema Mafuru.

error: Content is protected !!