Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tukio la Mbowe, Chadema wapinga taarifa ya Polisi
Habari za Siasa

Tukio la Mbowe, Chadema wapinga taarifa ya Polisi

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa (aliyesimama) akimjulia hali Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), limepinga taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu matokeo ya awali ya uchunguzi wa tukio la Freeman Mbowe, mwenyekiti wake, kushambuliwa na watu wasiojulikana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe anadaiwa kuvamiwa na kushambuliwa na watu watatu wasiojulikana usiku wa kuamkia tarehe 9 Juni 2020, nyumbani kwake Area D jijini Dodoma.

Kwa sasa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, ambapo ameshafanyiwa upasuaji katika mguu wake wa kulia.

Baada ya tukio hilo, Jeshi la Polisi kupitia David Misime, Msemaji wake, jana Ijumaa tarehe 12 Juni 2020, lilitoa taarifa ya matokeo ya awali, kuhusu uchunguzi wa tukio hilo.

Katika maelezo yake, Jeshi hilo limesema lina mashaka na maelezo ya mhanga (Mbowe),  ya kwamba alivamiwa na kushambuliwa na wasiojulikana, na kwamba, wakati wa tukio hilo, alipiga keleleza kuomba msaada.

Taarifa hiyo ya Misime ilidai, uchunguzi wa awali wa polisi, umebaini watu waliokuwepo eneo la tukio hilo (Mashahidi), hawakuona Mbowe akishambuliwa na wasiojulikana hao au kusikia kelele zake wakati anashambuliwa.

“Upelelezi wetu umepata ushahidi wa kutosha kwenye eneo la tukio unaonesha kulikuwa na watu ambao kwa namna yoyote wangeweza kusikia makelele yaliyopigwa na Mbowe kuomba msaada na wengine walikuwa ana uwezo wa kuona bila kizuizi itendo cha kushambuliwa,” inaeleza taarifa ya Polisi.

Hata hivyo, John Mrema, Mkurugenzi wa Uenezi, Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, amedai Jeshi la Polisi limesema uongo kuhusu tukio hilo.

“Kama ilivyokuwa tukio la kushambuliwa Tundu Lissu hadi tukataka wachunguzi wa kimataifa, wamerudia tena utaratibu huo wa kusema uongo. Imekuwa ni kawaida yao kuficha ukweli na kuzusha mambo,” amedai Mrema.

Mrema amelitaka Jeshi la Polisi kuendelea na uchunguzi wake ili kubaini ukweli juu ya tukio hilo.

“Tunalitaka jeshi la polisi lifanye majukumu yake kwa weledi na sio kujiingiza kwenye propaganda za kisiasa ambazo zitalifanya lisiaminike kwa wananchi,” amesema Mrema.

Lissu, Makamu mwenyekiti wa Chadema Bara, alishambuliwa na watu wasiojulikana mchana wa tarehe 7 Septemba 2017 kwa risasi zaidi ya 30 huku 16 zikimpata mwilini.

Tangu kutokea kwa tukio hilo, hakujawahi kukamatwa kwa mtu yeyote kutokana na tukio hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!