May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tukio la Adhana: Uhuru awakosha Waislam Kenya

Uhuru Kenyata, Rais wa Kenya

Spread the love

 

BARAZA la Waislam la Kenya (SUPKEM), limempongeza Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo, kwa kusimamisha hotuba yake wakati Adhana iliposomwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Tukio hilo na la aina yake, lilitokea juzi Jumatatu tarehe 22 Machi 2021, katika Uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma wakati wa kuaga kitaifa mwili wa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Wakati Adhana (wito wa swala kwa Waislam), ilipoanza kusomwa, Kenyatta ambaye alikuwa akiendelea kuhutubia wakati huo, ghafla alisimama kuzungumza na baada ya Adhana hiyo kumalizika, aliendelea na hotuba yake.

Tukio liligusa wengi na kupongezwa kwa Rais Kenyatta ambaye kiimani ni Mkristu kwa kutambua na kuthamini Imani za wengine.

Kwenye taarifa yake, SUPKEM limeeleza kuridhishwa na hatua ya Kenyatta kusimamisha hotuba yake kwa kupisha Adhana, kwamba ameupa heshima Uislam.

“Baraza la Waislam la Kenya linampongeza Rais Kenyatta kwa kusitisha kwa muda hotuba yake kwa kuheshimu Adhana,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Al-Hajj Hassan Ole Noado, mwenyekiti wa baraza hilo amesema, alichokifanya Kenyatta ndio utamaduni wa kiislam unaopaswa kufuatwa.

“Umeonesha heshima kubwa kwa Waislam na kufanya sisi viongozi wa SUPKEM kujivunia uongozi wako na umma wa kiislam wa Kenya kujivunia uongozi wako,” imeeleza taarifa hiyona kuongeza:

“Kwa niaba ya Waislam wa Kenya, tunachukua fursa hii kueleza kuthamini utawala wako na tunakuombea.”

error: Content is protected !!