May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tuisila Kisinda kuikacha Yanga, kutua Morocco

Spread the love

 

UONGOZI wa mabingwa wa kihistoria nchini Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam umesema, unakamilisha majadiliano na moja ya timu nchini Morocco kwa ajili ya kumsajili mchezaji wao raia wa Congo, Tuisila Kisinda. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Tuisila maarufu TK Master alijiunga na Yanga msimu wa 2020/21 akitokea AS Vital ya Congo.

Leo Jumatatu, tarehe 9 Agosti 2021, Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema, uongozi wa Yanga baada ya kupokea ofa hiyo na kuona muda wa mkataba wa Tuisila uliobaki “tukaona bora tukubali, fedha tukazozipata, zitumike kumtafuta mchezaji mwingine.”

“Ni kweli tulipokea ofa kutoka moja ya timu ya Morocco zikihitaji huduma ya mchezaji wetu Kisinda. Tupo katika biashara ya soka, ilikuwa ni ofa nzuri kwa mchezaji mwenyewe.”

“Tulizingatia na muda wa mkataba uliobaki na hii ni nafasi nzuri na baada ya kuweka mizania, tukikaa naye hadi mwisho wa msimu akaondoka akiwa huru,” amesema Mfikirwa

Katibu mkuu huyo amesema “unaweza kufanya ubishi wa kubaki naye, anaweza asicheze vizuri, tumewasiliana na mwalimu na tupo katika hatua za mwishomwisho kumalizana naye na tutasajili mwingine.”

error: Content is protected !!