Saturday , 3 June 2023
Home Kitengo Michezo Tuisenge arejea APR, asaini miaka miwili
Michezo

Tuisenge arejea APR, asaini miaka miwili

Spread the love

MSHAMBULIAJI raia wa Rwanda Jacque Tuisenge amesaini miaka miwili kuitumikia klabu ya Apr inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo akitokea klabu ya Petro Luanda ya nchini Angola. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea).

Mshambuliaji huyo ambaye aliwika na Gor Mahia ya nchini Kenya akitokea klabu ya Polisi kutoka nchini Rwanda, ameamua kurejea nyumbani mara baada ya kudumu kwa msimu mmoja na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Angola.

Tuisenge ambaye ni moja ya mshambuliaji mahili kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, amejipatia umaharufu akiwa nchini Kenya akiwa na klabu ya Gor Mahia ambayo alijiunga nayo januari 2016 akitokea nchini Rwanda na kufanikiwa kufunga jumla ya mabao 50 katika misimu minne aliyokaa hapo.

Kurejea kwake APR huenda ikaongeza chachu kwa timu hiyo katika kufanya vizuri kwenye michezo ya Ligi Kuu nchini humo na michuano ya kimataifa.

Mshambuliaji huyo alizaliwa 22 septemba, 1991 katika mji wa Gisenyi uliopo Rwanda alianza safari yake ya soka kwenye klabu ya Kiyovu Sport, na kisha kuelekea Police na baadae alifanikiwa kujiunga na Gor Mahia, 2019 alielekea nchini Angola kwenye klabu ya Petro Luanda na kurejea nyumbani kwenye klabu ya APR.  

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

error: Content is protected !!