December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tuhuma zamwandama Rais Magufuli

Spread the love

TUHUMA zimeendelea kuelekezwa kwa Rais John Magufuli kutokana na hatua yake ya kukwepa jukumu la kutatua mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar, anaandika Faki Sosi.

Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero (Chadema) amesema, hatua yake ya kuupa mgongo mgogoro huo inaashiria kuitenga Zanzibar.

Akizungumza na Mwanahalisi Online leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye uzinduzi wa programu ya kuwezesha umulikishaji Ardhi, amesema kuwa, hatua hiyo ni ‘utoto wa kisiasa’ na kwamba, yeye kama Raia wa Jamhuri ya Muungano hawezi kuepuka mgogoro huo.

Akiwa kwenye Mkutano na Wazee wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam wiki iliyopita, Rais Magufuli alisema kwamba, hatoingilia mgogoro huo kwa madai unapaswa kutatuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (NEC).

Kauli yake imepingwa na kada mbalimbali nchini zikidai kuwa, anachokifanya rais huyo ni kukimbia majukumu yake sambamba na kutaka kukiokoa chama chake (CCM) kilichoshindwa kwenye uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015.

Lijualikali amesema, kauli hiyo inaashiria uvunjifu wa Muungano kutokana na kuyatenga masuala ambayo angeweza kuwajibika kama amiri jeshi mkuu.

error: Content is protected !!