January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tuhuma za ngono, zamsimamisha Mhadhiri UDOM

Chuo Kikuu cha Dodoma

Spread the love

 

CHUO kikuu cha Dodoma (UDOM) nchini Tanzania, kimemsimisha kazi Mhadhiri wake, Petro Bazil Mswahili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za ngono kati yake na wanafunzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi, tarehe 28 Oktoba 2021 na kitengo cha uhusiano kwa umma na masoko wa UDOM umesema, Mswahili amesimamishwa tangu 25 Oktoba 2021.

Uamuzi huo umetangazwa baada ya siku za hivi karibuni, kusambaa mitandaoni kipande cha video na picha zikimwonesha mhadhiri huyo pamoja na msichana, anayedaiwa kuwa mwanafunzi wakiwa chumbani.

Katika video hiyo, inasikika sauti ikieleza mhadhiri huo amewapa ‘supp’ wanafunzi hususan wa kike na ili waweze kuwaondoa kwenye mkwamo huo wa mitihani yao, lazima wampatie rushwa ya ngono.

Katika taarifa hiyo ya UDOM imesema “Chuo kinapenda kuutaarifu umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote, chou kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote.”

error: Content is protected !!